Heshima za mwisho: Kutoka kushoto, Victor Valdes, Carles Puyol, Xavi na Andres Iniesta wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili wa Tito Vilanova
Wachezaji wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani.
Mkewe na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota, alilia sana.
Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia
Lionel Messi alikuwepo pia kumuaga Vilanova
Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45
"Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza.
Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo
Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana
Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.