Na. Paul Manjale
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney ameigia hofu baada ya klabu hiyo kuwa na mpango wa kumuajiri muholanzi Louis Van Gaal kama kocha wake mpya baada ya Timu hiyo kumtimua David Moyes.Hofu hiyo ya Rooney inatokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya kocha huyo na mshambuliaji muholanzi aliyepo klabuni hapo Robin Van Persie.
Rooney anahisi uwepo wa kocha huyo Manchester United utamrudisha katika kumbukumbu za msimu wa mwisho wa kocha Alex Ferguson.
Ambapo alishuhudia Robin Van Persie akiwa ndiye mshambuliaji chaguo la kwanza huku yeye (Rooney) akiwa chaguo la pili na nyakati flani flani akianzia benchi.
Tusubiri tuone kama mambo yatakuwa yaleyale ama tofauti itakuwepo..
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.