Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Hamis Kiiza akiipachikia timu yake bao la nne kati ya saba yaliyotiwa kimiani wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa hivi leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga imeshinda kwa Bao 7-0.Mshambuliaji wa Yanga,Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku mabeki wa timu ya Komorozine ya nchini Comoro wakimsindikiza wakati wa mchezo wao wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliochezwa hivi leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Yanga imeshinda kwa Bao 7-0.Mrisho Ngassa bado yuko na mpiraaaaa.....Mrisho Ngassa anapachika bao paleeeee...... Gooooooooo ni goli la sita hili lililofungwa na Mrisho Ngassa na kuwa mchezaji pekee aliefunga bao tatu peke yake.Wachezaji wa timu ya Komorozine wakilaumiana.
Mabingwa wa Tanzania, Yanga wameitembezea kipigo cha mbwa mwizi timu ya Komorozine de Domoni toka Comoro cha mabao 7-0. Mabao ya Yanga yametiwa kimiani na Mrisho Ngassa (13,65,68), Didier Kavumbagu (58,81), Cannavaro (20) na Hamis Kiiza (59).
Hongera sana Dar es Salaam Young Africans.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.