Unknown Unknown Author
Title: SHILOLE AMPA KITCHEN PARTY BABY MADAHA HEBU JISOMEE MWENYEWE HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya msanii wa Candy n Candy, Baby Madaha kufunguka akimchana wazi msanii mwenzake wa kike, Shilole aka Shishi Bybee kwa kudai kuwa nyim...

ShiloleBaada ya msanii wa Candy n Candy, Baby Madaha kufunguka akimchana wazi msanii mwenzake wa kike, Shilole aka Shishi Bybee kwa kudai kuwa nyimbo zake haziwezi kulinganishwa na nyimbo anazofanya Shilole, Shilole nae kakikalia kiti kile kile na kuyajibu makavu hayo.

Shilole amedai kuwa hawezi kupoteza muda kumzungumzia Baby Madaha, na kwamba yeye anaamini hana tatizo naye lakini anashangaa kuona anamzungumzia.

“Ni kama Baby Madaha anavyonizungumzia mimi, mmekua mkiona na wengine mliumia mkasema sana kwa nini ananizungumzia mimi. Baby Madaha sina tatizo naye lakini nashangaa amekuwa mtu wa kunizungumzia everyday, I don’t know why.” Amesema Shilole.

Mkali huyo aliamua kumpa ushauri Baby Madaha kwa kile alichokiita kumsema yeye vibaya ni kupoteza muda wake.

“Wewe mwanamke, mimi mwanamke mwenzio nafanya kazi, umeshaniona hata siku moja naenda kukuzungumzia somewhere? Muogope Mungu kukaa unamzungumzia mtu ambaye hana time, hana shida na wewe. Hebu tubadilike wanawake tupendane tuache kuzumziana vibaya.” Shilole ameeleza.

“Kwani ukinizungumzia mimi vizuri utapata nini, najua kuna vitu vingi nimekuzidi lakini usikae unamzungumzia vibaya. Wanawake tupendane tupeane sapoti. Ndio maana hatufiki mahali tunabaki tu kulalamika ‘ooh nimerogwa’, hujarogwa umejiroga mwenyewe.” Shilole anakaririwa.

Chanzo: Channel 10

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top