Unknown Unknown Author
Title: WAZIRI AWASHUSHA VYEO OFISA ELIMU, NA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI MBINGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa (pichani), ametengua uteuzi wa Ofisa Elimu ya Sekondari wa Wila...

Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa (pichani), ametengua uteuzi wa Ofisa Elimu ya Sekondari wa Wilaya ya Mbinga, Hanji Godigodi na wakuu sita wa shule za sekondari wilayani humo kwa tuhuma za ubadhilifu Sh60 milioni.KASIMU MAJALIWAPamoja na kutengua uteuzi huo pia amewaagiza maofisa hao wa elimu wachukuliwe hatua mara moja.

Majaliwa alitangaza hatua hizo juzi alipokuwa akizungumza na walimu wa shule za msingi na sekondari, mjini Mbinga.

Katika mazungumzo yake, alimtuhumu Ofisa Elimu ya Sekondari wa Wilaya ya Mbinga, kuwa amekuwa akishirikiana na baadhi ya wakuu wa shule za sekondari, kutafuna fedha za ruzuku, zinatolewa na Serikali kwa ajili ya kununulia vitabu.

Alisema fedha hizo zimekuwa zikiliwa kwa njia ya kugawana posho, jambo ambalo alisema ni ukiukwaji wa sheria.

Aliwataja wakuu wa shule ambao vyeo vyao vimeshushwa kuwa ni Leonard Juma, William Hyera, Clemence Sangana, Method Komba na John Tillia.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, nafasi za wakuu hao sasa zinachukuliwa na walimu wakuu wasaidizi ambao barua za kupandishwa madaraja zitatumwa mara moja.

Alivitaka vyombo vya usalama kumchunguza ofisa elimu huyo na kumchukulia hatua za kisheria.

Alisema kamwe Serikali haiwezi kuvumilia vitendo hivyo.

“Nimekwazwa sana na kitendo cha ofisa elimu kushirikiana na wakuu wa shule kutumia fedha za maendeleo, kulipana posho,” alinena.

credit to MWANANCHI

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top