Arsene Wenger jana alipatwa na majanga mawili ya mwaka baada
ya kula mweleka muda mfupi baada ya timu yake ya Arsenal kupigwa 5-1 na Liverpool. Meneja huyo wa washika bunduki wa Uingereza alikuwa anawahi treni kurudi London katika mtaa wa Lime jijini Liverpool akiwa na wachezaji wake alipoteleza na kuanguka pwa!
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 64 anaokenana pichani akiwa anaburuta begi lake wakati akiingia stesheni, lakini mara tu
baada ya kuvuka mlango wa kuingilia, anateleza na kula mweleka.
Mfaransa huyo aligumia kwa maumivu wakati askari polisi wawili walipofika kumsaidia. Msemaji wa Arsenal alinukuriwa baadaye
akisema kuwa mzee mzima hakuumia na hajambo.
Kama ulipitwa na Mechi hiyo Tazama Hapa Magoli hayo::
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.