MTOTO WA MGIMWA ASHINDA KURA ZA MAONI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA

mgimwaGodfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi ya baba yake kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa.

Na Francis Godwin, Iringa

Mtokeo ya kura za maoni ndani ya CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo huku mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa kishindo katika nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.

Godfrey Mgimwa amepata kura 342 huku Kiswaga akipata kura 170 na mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia kura 42 .

Matokeo hayo yaliyotangazwa katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwembetogwa mjini Iringa yanaonesha mgombea Peter Mtisi kapata kura 33, Msafiri Pangagira kura 8, Bryson Kibasa kura 7, Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post