Tanzania. kama kawaida, leo Tutakuletea mwenendo mzima wa uchaguzi wa udiwani katika kata 27 nchini ambapo wananchi watapiga kura kuwachagua madiwani wao kwenye kata hizo.
Tutawaletea matukio kwenye kata hizo, hasa Kata ya Sombetini ambayo imevuta hisia za watu wengi kutokana na kata hiyo kuwa katika mkoa wenye ushindani mkubwa wa kisiasa.
Pia matokeo ya kura, kama vurugu zitatokea au kuibwa kwa kura- yote hayo tutawajulisha kupitia lindiyetu.com.
Updates
Source; Mwananchi BreakingNews.
Kata ya Kiwalala Mjini Lindi, Wananchi wameendelea na Zoezi la Upigaji kura kwa hali ya Usalama na Kufuata taratibu zote zilizowekwa na Tume ya uchaguzi, Hakuna Tatizo lililojitokeza hadi Sasa
Updates ArushaMmoja ya wapiga kura katika Kata ya Sombetini Arusha, akivutana na polisi HIVI PUNDE baada ya kutimiza haki yake. Polisi walikuwa wanamtaka akae mbali na eneo la kupigia kura.
UPDATES
WAKATI Chama Cha Mapinduki (CCM),ikishinda Kata 24 Kati ya Kata 27 ambazo Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Umefanyika jana Kote Nchini, mjini Kigoma katika jimbo la Mbunge wa Chadema Zitto Kabwe ushindi umekwenda kwa CCM.
Hatua ya Chadema kushindwa katika kata ya Mkongoro inatokana na mgogoro ulioikumba Chama hicho baada ya Mbunge huyo kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama hicho.
Mchanganuo wa matokeo hayo katika baadhi ya kata kwa ufupi
KUTOKA BAGAMOYO KIBINDU. Matokeo ya jumla: CCM- kura 1682(75%),CHADEMA- kura 548(25%).
MAGOMENI :Matokeo kwa jumla: CCM 1183, CUF 708, CHADEMA 347.
KUTOKA LINDI NA MTWARA. CCM imeshinda Kata Zote za Uchaguzi Uliofanyika jana .
NACHINGWEA. ...ADC -9 CUF -110 CHADEMA -188 CCM -517.
KUTOKA KIGOMA JIMBONI KWA ZITTO KABWE: CHADEMA wamepoteza kata ya MKONGORO Jimboni KWA Zitto Kabwe,Imechukuliwa na CCM(Kata Ilikuwa Inaongozwa na CHADEMA).
KUTOKA MOSHI. Kata ya Kiboroloni imebakia CHADEMA
KUTOKA KONDOA: CCM --1,296 CUF--935. CDM--29 NCCR—34
KUTOKA SOMBETINI JIJINI ARUSHA: CHADEMA Imeshinda Kata ya Sombetini kwa 2548 na CCM 2077
KUTOKA RUNGWE MKOANI MBEYA: CCM Imeshinda kata ya Malindo na Matokeo rasmi Kata ya SANTILYA-Mbeya Vijijini. CCM - 1650 CDM - 1154.
KUTOKA MANYARA KITETO: CCM Imeshinda kata Zote mbili ikiwamo ya Partimbo.
KUTOKA KAHAMA KIBAGWE: CCM Imeshinda Kata ya Kibagwe (kulikuwa na Kata moja tu ya Uchaguzi).
KUTOKA BUNDA: CCM Imeshinda (Kulikuwa na Kata Moja ya Uchaguzi)
KUTOKA NJOMBE MJINI:: Chadema Imeshinda ( Kata Ilikuwa Moja tu ya Uchaguzi).
KUTOKA LUDEWA :CCM imeshinda,Kulikuwa na Kata Moja ya Uchaguzi.
Hitimisho: Katika kata 27 zilizofanyiwa Uchaguzi,CCM Imeshinda kata 24,Chadema Kata 3. Kwa Maana hiyo CCM Imeshinda Kwa Kishindo Uchaguzi huu hasa Ukizingatia UShindani wa Kisiasa Uliokuwepo siku za hivi Karibuni..
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.