Unknown Unknown Author
Title: MASAI NYOTAMBOFU AKERWA NA TAARIFA ZA UZUSHI ZA KIFO CHA MCHEKESHAJI MWENZAKE BABA KUNDAMBANDA, SOMA ALICHOKISEMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
' Masai Nyotambofu ' Comedin at VITUKO SHOW Channel ten. Mcheshaji maarufu hapa nchini anatamba katika tasnia hiyo ya Vichekesho kw...

clip_image002[6]'Masai Nyotambofu' Comedin at VITUKO SHOW Channel ten.

Mcheshaji maarufu hapa nchini anatamba katika tasnia hiyo ya Vichekesho kwa lafudhi ya kabila la Wamasai, Gilliady Severine almaarufu 'Masai Nyotambofu' ambaye pia ni mmiliki wa Website inayotambulika kwa jina la masainyotambofu.com Leo amefunguka kukerwa na tabia ya baadhi ya watu kuwazushia wasanii vifo.

SOMA ALICHOKISEMA HAPO CHINI...

'Baba Kundambanda' (Mapembe) Kabla ya kuugua

KWAKWELI inasikitisha sana kwa tabia iliyozuka sasahivi ya kuwazushia wasanii kifo.! Yani mpaka sasa imetimia mwezi na ushee watu wanaungurumisha simu kwetu sisi wasanii wa VITUKO SHOW kwamba msanii huyu hapa pichani kafa!

HIVI kwanini mtu ukipewa taarifa usiifanyie uchunguzi wa kina kabla haujaisambaza? Huyu ni msanii mkongwe na anafahamika na yupo kwenye kampuni haiwezekani afe kama panya kimyakimya mwezi mzima asitangazwe na
media yeyote jamani, Watu wengine bwana? Yani kila siku mapembe anakufa..! Mwezi mzima yeye kazi yake ni kufa tuuuuuuuuuu kuanzia asubuhi mpaka jioni anakufa...! Jamani mlinitangazia mimi eti nimejinyonga hautosha mkamtangazia masele kuwa kafa miezi miwili tunapokea simu za msiba..! Au mna hamu ya kuzika?

Hebu wenye tabia hio badilikeni jamani mnakera sana maana mnatutesa sisi Simu zetu zinakuwa ni zakupokea simu za misiba tuuuuuuuuuuu kila kukicha na ilhali mtu mwenyewe yuko hai ispokuwa ameumwa tu kwa mda mchache na kuumwa sio kufa.

Kibaya zaidi wanadiriki kumpigia yeye mwenyewe na kumuuliza eti tunaambiwa umekufa hivi we uliopokea simu hii ni wewe kweli? Ukizingatia amepata nafuu lakini hajapona kabisakabisa kwani ugonjwa ni rahisi kuingia lakini kutoka ni mbinde,

Kwahio nawaomba jamani watu wangu wa nguvu mkisoma habari hii mushee na kwe wengine wasome ili kupunguza usumbufu huu uliompelekea Baba Kundambanda kuzima simu yake matokeo anawapa ndugu zake wasiwasi wakiongea na sisi kwenye simu zetu hawaamini wanahisi kuna jambo tunaficha kutokana na taarifa wanazozipata kila dakika.

Watu wetu wa KUSINI. LINDI, MASASI, MTWARA NZIMA kwa ujumla msijali wala msiwaze Baba Kundambanda ni mzima anaendelea vizuri, tumuombee mungu kwa pamoja ili apate nguvu mapema arudi kazini maana najua wadau mmemisi ladha yake.

clip_image002'Baba Kundambanda' (Mapembe) Sasahivi baada ya kuumwa.

Yuko safi siku sio nyingi anakaria kuingia kazini kama kawaida kwa uwezo wa mwenyezi mungu.


About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top