Unknown Unknown Author
Title: MADIWANI 13 WASUSIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI, WAJIORODHESHA KUMKATAA MEYA WAO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MADIWANI 13 Wa Manispaa ya Lindi wametoka nje ya ukumbi wa kikao cha baraza la madiwani leo hii wakigomea kikao hicho kutokana na kuchoka ku...

madiwaniMADIWANI 13 Wa Manispaa ya Lindi wametoka nje ya ukumbi wa kikao cha baraza la madiwani leo hii wakigomea kikao hicho kutokana na kuchoka kuburuzwa na Meya wa Manispaa wa Lindi kwa kutosikiliza ushauri wao na kuwahusisha katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.madiwani.9Madiwani hao wametoka nje kufuatia sakata la Mradi wa UTT wa ugawaji wa Viwanja ambao unalalamikiwa na wananchi waliochukuliwa maeneo yao kwa kurudishiwa gharama hafifu ukilinganisha na Thamani ya Ardhi hiyo na ardhi hiyo kuuzwa kwa bei ya juu.

Madiwani hao walifikia hatua hiyo ya kutoka nje baada ya Meya wa Manispaa kutosikiliza Hoja yao ya kuanza kusikiliza Hoja hiyo ya Mradi na badala yake Meya aliendelea na Kufuata kanuni za kikao chakawaida cha Baraza hilo cha kila baada ya Miezi mitatu na Ndipo Madiwani 13 Pamoja na Waheshimiwa Wabunge 2 walio hudhuria kikao hicho walisimama na Kutoka nje ya ukumbi wa Mikutano wa Manispaa hiyo wa DDC na Kutoa mmsimamo wao juu ya Mstakabali wa Hoja yao ya Msingi.

Sasa waahidi kujiorodhesha kumkataa Meya Wao Frank Magali kwa kutokuwa na Imani nae.

madiwani.2Mh.barwan akiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya Kutoka Katika Ukumbi wa Kikao cha Baraza la madiwani ambacho madiwani 13 walitoka nje kwa kususia kikao hicho.madiwani.3Diwani wa Kata ya Mingoyo Ndg Jamaldin Mandowa akizungumzia msimamo wao na kwanini wameamua kutoka nje kususia kikao hicho cha Baraza la madiwani cha Kila Miezi Mitatu kama kilivyoitishwa na Mh. Meya wa Manispaa ya Lindi. madiwani.8Mbunge wa Viti maalum CCm jimbo la Lindi Ndg Lulida akiongea na waandishi wa Habari naye ameungana na Madiwani wengine katika kutokuwa na imani na Mh. Meya wa manispaa ya lindi kwa Jinsi Mambo yanavyo kwenda kuhusiana na Mradi wa UTT. madiwani.6Mmoja wa Wahanga waliokubwa na Majanga ya Kuchukuliwa Ardhi katika eneo la mradi akionesha vitabu vyake alivyotumia kununulia ardhi hiyo lakini ni Tofauti na Gharama aliyolipwa na Manispaa ya Lindi katika Mradi huo wa UTT.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top