Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi(LPC) Inatoa Pongezi kwa ACP Renatha Mzinga aliekuwa Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi kwa kuteuliwa na MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa LINDI.
Taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi, Abdulaziz Ahmeid ameeleza kuwa Klabu hiyo Imepokea mabadiliko hayo na kuhaidi Ushirikiano mkubwa baina ya klabu na Jeshi hilo.
"Kwa niaba ya wanahabari nampongeza Mkuu wa Jeshi hilo IGP Mangu kwa uteuzi huu nasi tutamuunga mkono katika kazi zetu za kila siku kwa kuwa kwa kipindi kifupi alichokuwapo Lindi Tumeona Ushirikiano wake kwa wanahabari kwa kujadiliana na kuwa huru kutoa habari Isitoshe tumeshuhudia alivyoweza kuwaunganisha Polisi na kujua baadhi ya Changamoto zao hususan Alivyowaunganisha askari wa kike(WP) Katika kuunda mtandao wa polisi wanawake hali iliyoonekana ni mabadiliko makubwa”
Hivi karibuni Kamanda Renatha alifanikisha zoezi la Usafi na kutoa
misaada kwa kituo cha walemavu kilichopo Manispaa ya Lindi na askari hao kushiriki kutoa walichonacho kusaidia walemavu hao.
Waandishi wa habari hufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo hivyo
tunatarajia kupata Ushirikiano mkubwa toka kwa Kamanda Mzinga na
wasaidizi wake wakati wa matukio ya dharura na yasiyo ya dharura na kuondoa hali ya Polisi wachache kuona Waandishi wa Habari ni maadui wakubwa kutokana na maovu yao.
Mwaka jana Klabu ya waandishi wa habari ilifanya kazi vizuri na Jeshi
hilo na Kufahamu wana habari,,
Ilimalizia taarifaa LPC Iliyotolewa na Mwenyekiti wake Abdulaziz
Ahmeid ambae pia ni mwandishi wa Channel ten mkoa wa Lindi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.