Unknown Unknown Author
Title: HUU NDIO UPENDO WA JOSE CHAMELEONE KWA FAMILIA YAKE, AJICHORA TATOO YENYE JINA LA MKEWE NA WATOTO WAKE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakati tunaelekea katika ile siku inayoaminika kuwa siku ya wapendanao ‘ Valentine’s Day’ , mkali wa Valuvalu Jose Mayanja Chameleone ameamu...

Wakati tunaelekea katika ile siku inayoaminika kuwa siku ya wapendanao ‘Valentine’s Day’, mkali wa Valuvalu Jose Mayanja Chameleone ameamua kumuonesha mkewe Daniella na dunia nzima jinsi anavyompenda, kwa kujichora tattoo yenye jina lake shingoni.josekamilioniChameleone ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa shughuli za kimuziki, alipost picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, picha zinazoonesha tattoo hiyo hata mtu akimuona kwa mbali kidogo.

Mwimbaji huyo wa Valuvalu ambaye ana watoto watano aliozaa na mkewe Daniella hakuwasahau wanae pia, alijichora katika mkono wa kushoto tattoo yenye majina manne ya wanae wanne na anatarajia kuongeza moja yenye jina la mwanae wa kwanza, Ayla.

“2014 we stand tall for the ones we care for and those that love us back with their whole. For me, this is my expression..” Amesema Chameleone.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top