Mwenyekiti wa mwavuli wa asasi zisizo za kiserikali mkoa wa Lindi,Bw
Muzihir Mewileakifungua mdahalo wa mabadiliko ya tabia Nchi katika
ukumbi wa Leinas Liwale
Liwale..
Wananchi wilaya ya Liwale mkoani Lindi wametakiwa kuhifadhi na kulinda misitu na kuacha tabia ya kulima kwenye vyanzo vya maji na kukata miti ovyo ili nchi hisiwe jangwa.
Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Lindi( LANGO)Mudhihiri Mewile wakati alipokuwa anafungua mdahalo kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika ukumbi wa raines mjini Liwale.
Mewile alisema tabia inayoendelea hivi sasa ya ya kuvamia misitu kwa
ajili ya kilimo cha ufuta na kulima kwenye vyanzo vya maji
itasababisha nchi kuwa jangwa na kutishia uhai ya viumbe na ongezeko la joto katika uso wa dunia.Alisema kuwa licha ya kuwepo kwa matokeo hayo pia uharibifu huo
utachangia kushuka kwa pato la mwananchi na taifa na kusababisha
ugumu wa maisha kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa mazao ya
chakula na biashara.
Mewile aliwashauri wananchi kuacha tabia ya kuchoma moto ovyo ili
kuinusuri misitu na viumbe wengine kukosa vivuli, maeneo salama ya
kuishi na chakula kutokana na kupotea nyasi.
Alisema kuwa ipo tabia ya wakulima kutumia kilimo cha kizamani cha
kuhamahama, kinachangia uharibifu mkubwa wa mazingira, pamoja na kupunguza nguvu za wakulima kutokana na kukata miti kila mwaka kwa ajili ya maandalizi ya shamba jipya badala ya kulima eneo moja na kutumia pembejeo.
Kwa upande wake mwenzesha wa mdahalo huyo Nyaindi Stephen alisema mabadiliko ya tabia ya nchi ni ya muda mrefu na huathili maisha ya binadamu katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kimazingira, afya kutokana na ongezeko la hewa ukaa.