NA. ABDULAZIZ, LINDI
Mkuu wa wilaya Lindi Dk Nasoro Hamid amewataka wananchi
wilayani humo kudumisha amani na utulivu na kuacha tabia ya kushabikia mambo yanayoweza kuchangia kuvunja umoja na ushikamano uliopo.
Wito huyo ameutoa wakati alipokuwa anazungumza na waislamu kwenye sherehe za kuazimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mtume Mohamed (s,w,a) ambayo kila mwaka ufanyika mwezi 12 mfungo sita kiarabu, yaliyofanyika uwanja wa Ilulu.
Dk hamidi alisema kuwa ni wajibu wa jamii kutambua kuwa amani na
utulivu wa nchi yetu umetokana na umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wa nchi ambao hautakiwi kuchezewa na mtu, kikundi, taasisi wala vyama vya siasa.
Alisema ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda amani na utulivu huo ili
nchi yetu iendelee kutukuka kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu japo
wapo baadhi ya watu, na vikundi vimeaanza kutaka kuharibu sifa hiyo.
Dk hamidi aliongeza kwa kuwataka viongozi wa dini zote wilayani humo kutoa elimu ya maadili kwa waumini wao ili kuepuka mmomonyoko wa maadili kwa jamiii.
Alisema kuwa kuna mambo mbalimbali yameanza kujitokeza katika jamii yetu kama vile kuvaa nguo fupi zinaonyesha maumbile kwa watoto wakike, watoto wa kiume kuvaa eleni na kusuka nywele ambayo sio utamaduni wa kitanzania.
Dk hamidi alisema kuwa mambo hayo yanachangia ushawishi wa ngono zembe na kusababisha kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi na kupoteza nguvu kazi katika jamiii.