Unknown Unknown Author
Title: VUGU VUGU LA MECHI YA WATANI KARIAKOO FC Vs KUSINI SOCCER, MGANGA APOTEA GHAFLA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtu mmoja amepotea katika mazingira ya kutatanisha mjini lindi na hadi sasa hajaweza kupatikana. Mtu huyo ameweza kuhusishwa katika imani z...

clip_image001Mtu mmoja amepotea katika mazingira ya kutatanisha mjini lindi na hadi sasa hajaweza kupatikana.

Mtu huyo ameweza kuhusishwa katika imani za Kishirikina katika Mchezo wa Soka katika Ligi ya Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa Mkoani Lindi kwa kusemekani ni Mganga wa Timu (jina kapuni).

Baada ya mechi hiyo Kuahirishwa hapo jana alionekana Maeneo ya Mjini huku akiweza kuishutumu timu hiyo kwa kumtelekeza tangu afike mjini hapa huku wakishindwa kumlipia hata nauli yake aliyoitumia wakati anasafiri kutoka katika makazi yake hadi mjini lindi na kusema kuwa hata chakula alikuwa hajala….Kilisema chanzo hicho.

Katika kupata ukweli wa Jambo mwandishi wetu aliwasiliana na kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Ndg G. Mwakajinga kuthibitisha kuwepo kwa taarifa za utekwaji wa mtu huyo lakini kamanda huyo alithibitisha kuwa zipo taarifa za kupotea kwa mtu lakini haijathibitika kwamba ametekwa au la…

kwani taarifa hizo zinahusishwa na mpira zaidi hivyo yawezekana amewekwa mahali na mpira utakapo malizika mtu huyo anaweza onekana, lakini Polisi wanaendelea na Uchunguzi wa Taarifa Hizo.

Hadi sasa watu kadhaa wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za Kupotea mtu huyo..

Endelea kuwa nasi kwa Kupata

UPDATES ZA MECHI HIYO KUANZIA SAA KUMI KAMILI LEO JIONI UWANJA WA ILULU (BOFYA HAPA )

KARIAKOO FC Vs KUSINI SOCCER (LINDI DERBY)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top