UNAHISI HII ITAKUWA COLABO BORA KULIKO? PROF. JAY & DIAMOND PLATNUMZ #PRODUCED BY P FUNKY

Msanii mkongwe katika game ya Bongo Fleva Joseph Haule (Prof. Jay) ambae amesababisha ushawishi mkubwa sana kwa kijana kuingia kwenye game hii na hata baadhi ya wazazi kuelewa muziki huu.clip_image001Kupitia kurasa yake ya Facebook Jay amepost picha akiwa katika studio za Bongo Records inayomilikiwa na Producer mkongwe nchini Tanzania P. Funk Majani wakiwa pamoja na Diamond Platinum.
Amepost picha hiyo pamoja na maneno haya "Ndani ya Bongo Records with the Super dupa producer P - funk Majani and @diamondplatnumz himself Muda Huu # COOKING for all yall'.... kaeni mkao wa kula watu wangu!!!"
Hivyo kuna kila dalili ya kuwepo collabo ya wawili hao ambayo inapikwa na P. Funk, vuta picha itakuwaje Msanii mkongwe + Producer Mkongwe + Msanii anaevuma zaidi kwa sasa = Jibu unalo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post