Unknown Unknown Author
Title: SIMBA NA KCC KUCHUANA LEO KATIKA FAINALI YA MAPINDUZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Fainali ya kombe la mapinduzi inatarajiwa kupigwa leo saa 10 alasiri katika uwanja wa Amani kisiwani Unguja kwa kuwakutanisha mabingwa wa mw...

clip_image001Fainali ya kombe la mapinduzi inatarajiwa kupigwa leo saa 10 alasiri katika uwanja wa Amani kisiwani Unguja kwa kuwakutanisha mabingwa wa mwaka 2011 wa kombe hilo Simba SC dhidi ya wageni wa mashindano hayo timu ya KCC.

Mchezo huo wa fainali unazikutanisha timu ambazo zilikutana katika hatua ya makundi wakiwa katika kundi B, ambapo walipokutana mchezo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Simba SC ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kutokana na kuwa na safu bora ya ulinzi katika mashindano hayo ambapo mpaka kufikia hatua ya fainali bado hawaja ruhusu nyavu zao kuguswa huku safu yake ya ushambuliaji ikifanya kile kinachotakiwa kufanya.

Kwa upande wa KCC ambao wametinga fainali kwa kumvua ubinga Azam FC ambayo nayo kabla ya kukutana na KCC walikuwa hawajaruhusu nyavu zao kuguswa.

Nnje ya kuwaondosha mabingwa watetezi pia KCC waliwaondosha makamu bingwa wa mwaka jana Tusker kwa mikwaju ya penati, hivyo kupelekea mchezo wa leo kuwa mgumu kwa Simba SC.

Simba SC katika hatua ya robo fainali wao waliondosha Chuoni kabla ya kuwaondosha URA ya Uganda kwa ushindi wa goli 2-0.

KCC na Simba SC hawakupoteza mchezo wowote ule katika hatua ya makundi ambapo walikuwa na timu ya KMKM pamoja na AFC Leopards katika kundi lao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top