Ule mtanange uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na washabiki lukuki wa timu zote mbili ili kuamua nani atakae ongoza ligi hiyo ya Daraja la Tatu ngazi ya Mkoa.
Wachezaji wa Timu ya Kusini Soccer wakipasha kabla ya Mechi Kuahirishwa leo jioni
Timu hizo pinzani katika mji huu wa Lindi zimetokea kuwa na ushindani mkubwa katika soka kupelekea fans wake kuwa na ubishi wa hapa na pale hivyo mechi hiyo ilikuwa ni kiu kubwa kwa wakazi wa mji huu ilikukata mzizi wa fitini kuwa nani mkali dhidi ya mwingine.
Wachezaji wa Kariakoo Fc wakipasha misuli kabla ya mechi yao dhidi ya Kusini Soccer kuahirishwa leo jion
Lakini mechi hiyo iliingia dosari kubwa pale Neema ya Mwenyezi mungu ilivyoshuka kwa wakazi wa mji wa Lindi na Vitokoji vyake kwa Kunyesha Mvua kubwa ambayo ilipelekea Uwanja wa ILULU kujaa maji hivyo kupelekea mechi hiyo kuahirishwa hadi siku ya kesho.
Refa akiwa na wasaidizi wake pamoja na Mechi kamishan wakijadiliana nini cha kufanya baada ya kuona jinsi uwanja ulivyo kuwa umetota maji yaliyo sababiswa na mvuakubwa ilionyesha leo hii mjini Lindi
Timu zote zilikuwa ziko uwanjani tayari kwa mchezzo huo lakini waamuzi viongozi wa chama cha mpira lindi pamoja na makocha wa pandi zote mbili walikubaliana mechi hiyo kuahirishwa kwani ingepunguza burudani kwa Watazamaji kutokana na Uwanja huo Kutota maji.
Ndg Khalfani Ibrahim Mwaya akitoa maelekezo jinsi ya utaratibu waugawaji wa Tiketi kwa aijili ya kesho.
Watazamaji waliokuwa wamesha kata Tiketi zao na kuingia uwanjani waripewa tiketi za ziada tena kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itarudiwa kuchezwa kesho saa 4:00 EAT katika Uwanja wa ILULU mjini Lindi.
Utaratibu ulizingatiwa na watazamaji woote walipatiwa tiketi na kuondoka salama uwanjani hapo kusubiri siku ya kesho.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.