Unknown Unknown Author
Title: KESHO NDIO KESHO BALLON D’Or:: RONALDO APEWA NAFASI KUBWA KUTWAA TUZO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
JUMATATU Usiku, kuanzia Saa 1 na Nusu, huko Kongresshaus, Zurich, Nchini Switzerland, mmoja kati ya Cristiano Ronaldo, Franck Ribery na Lion...

clip_image001JUMATATU Usiku, kuanzia Saa 1 na Nusu, huko Kongresshaus, Zurich, Nchini Switzerland, mmoja kati ya Cristiano Ronaldo, Franck Ribery na Lionel Messi ndio atatwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, 2013 Ballon d'Or.clip_image001[7]Wachezaji hao watatu walifuzu kuingia Fainali toka Listi ya Wagombea 23 na Mshindi kati yao atatangazwa kesho Januari 13 katika Hafla maalum.

Washindi wa Tuzo hizi hupatikana kutokana na Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa Wanachama wa FIFA pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari toka Dunia nzima wanaoteuliwa na Jarida la Soka la Ufaransa France Football.clip_image001[5]Kwa upande wa Kinamama, Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora ni Nadine Angerer (Germany), Marta (Brazil) na Abby Wambach (USA).

Kocha Bora atachaguliwa kutoka Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, Kocha wa zamani wa Munich Jupp Heynckes na yule wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp.

France Football ndio walioanzisha Ballon d'Or Mwaka 1956 ili kumpata Mchezaji Bora Ulaya na Staa wa England, Stanley Matthews, ndie alikuwa Mshindi wa Kwanza.

Mwaka 2007, Ballon d'Or iligeuka kuwa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani na kuanzia Mwaka 2010 ikawa FIFA Ballon d'Or na Mshindi wake ni Messi tangu wakati huo.

Safari hii, baada ya kuitwaa Ballon d'Or Mwaka 2008 akiwa na Manchester United, Cristiano Ronaldo, ndie anaetegemewa kumpiku Messi ambae ameitwaa mara 4 mfulizo hadi 2012.

Wakati Ribery akitegemea mafanikio yake na Klabu yake Bayern Munich yatamfanya afuzu, Ronaldo anategemea sana Rekodi yake binafsi ya kupiga Bao nyingi ndio itampa Tuzo hiyo.

Na hilo linampa nguvu Ronaldo kwani Tuzo hii ni ya Mchezaji binafsi na si Timu na Goli zake 66 katika Mechi 56 kwa Klabu yake na Nchi yake kwa Mwaka 2013 ndivyo vitakavyompa nguvu Ronaldo kutamba.clip_image001[9]Kawa upande wa Makocha, Jurgen Klopp atachuana na Makocha Magwiji wawili waliostaafu Mwaka 2013, Sir Alex Ferguson wa Manchester United baada kuiongoza Klabu hiyo kwa Miaka 27 na Jupp Heynckes alieifanya Bayern Munich itwae Trebo Mwaka Jana.

Kwa upande wa Kinamama, Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora ni Nadine Angerer (Kipa toka Germany), Marta (Brazil), ambae ameshaitwaa Tuzo hii mara 5 kati ya Mwaka 2006 na 2010, na Abby Wambach (USA) ambae alitwaa ile ya Mwaka 2012.MANDELA NA EUSEBIOWakati huo huo, Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amethibitisha kuwa katika Hafla hii ya Ballon d'Or heshima maalum kwa Kiongozi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, na Lejendari wa Benfica na Portugal, Eusebio, waliofariki hivi karibuni, zitatolewa.

Eusebio alitwaa Ballon d'Or Mwaka 1965.

TUZO ZITAKAZOTOLEWA Jumatatu Januari 13:

FIFA Ballon d’Or

FIFA Mchezaji Bora Kinamama

FIFA Kocha Bora Timu za Wanaume

FIFA Kocha Bora Timu za Wanawake

FIFA Tuzo ya Rais

FIFA Tuzo ya Uchezaji wa Haki

FIFA Tuzo ya Puskas [Goli Bora]

FIFA/FIFPro Kombaini ya Dunia [Kikosi Bora cha Wachezaji 11]

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top