Christopher Lilai, Nachingwea,
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Nachingwea, mkoa wa Lindi kimemsimamisha Katibu wake, Jordan Membe kwa madai ya kushiriki kusambaza waraka unaotaka
wajumbe wa baraza la uongozi la chama hicho kusaini ili kuwashinikiza viongozi wakuu wa Kitaifa waitishe baraza la uongozi haraka kuhusiana na mgogogro wa Zito Kabwe na wenzake.
Kufuatia hatua hiyo ambayo ilizua mvutano mkubwa kwenye kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika ijumaa huku baadhi ya wajumbe wakipinga kusimamishwa kwa katibu huyo hali iliyosababisha Mwenyeviti wa Kata 13 na makatibu wao wajihudhuru na mjumbe wa Baraza la wazee la wilaya Habaki Selemani kutishia kuwatimua kwenye nyumba yake ambamo ndimo zilimo ofisi za Chama hicho wakipinga hatua hiyo ya kumsimamisha Katibu huyo na nafasi hiyo kukaimishwa katibu wa BAVICHA Lauce China.
Habari ambazo zilipatikana kutoka miongoni mwa wajumbe waliokuwa ndani ya kikao hicho ilielezwa kuwa Membe amesimamishwa kuendelea na nafasi hiyo ya utendaji kwa
madai kuwa alikuwa ameshiriki kusambaza waraka ambao unamtaka Katibu mkuu wa chama hicho, Wilbrod Slaa kuitisha kikao cha Baraza kuu ili kujadili mgogoro unaondelea baina ya Chama hicho na aliyekuwa Naibu katibu Mkuu Zitto Kabwe na wenzake.
Chanzo hicho cha habari ambacho hakikutaka jina lake liandikwe gazetini kilieleza kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya wajumbe kuhusiana na kusimamishwa kwa Katibu huyo kiasi cha wajumbe 9 kati ya 13 waliokuwemo kwenye kikao hicho kukataa
kupiga kura kwa madai kuwa hawakuona sababu za msingi za kumsimamisha Membe.
Akizungumzia uamuzi huo wa kumsimamisha Membe alikiri kuwa
kamati ya utendaji imemsimamisha kwa kile alichokiita kuwa ni tuhuma za kupikwa kwani anadai hakuwahi kuuona waraka huo anaodaiwa kuusambaza na kubainisha kuwa mwenyekiti wake, Ahamadi Likolovela ndiye aliyekiri kwenye kikao cha kamati ya utendaji iliyoketi mwishoni mwa mwaka jana kuwa alisaini
waraka huo na kuwa hizo ni njama za kumuondoa kwa kisingizio cha
kuwa yupo kambi la akina Zitto.
“Mimi sihusiki kuusambaza waraka huo na sikuwahi hata kuona na hata kwenye kikao cha kilichofanyika mwezi uliopita nilikataa katakata kuhusika na waraka huo ila mwenyekiti wetu ndie alikiri mbele ya kamati ya utendaji kuwa alisaini na aliomba radhi sasa iweje wanihusishe …najua hii na njama yao ya kuniondoa” alisema Membe.
Wakati hali ikiwa hivyo Kaimu katibu wa wilaya ambaye amekaimishwa nafasi hiyo, Lauce China ameiandikia kamati ya utendaji barua ya kujihudhuru nafasi hiyo kwa madai kuwa hapendi kuwa sehemu ya mgogoro kwani alisema kuwa kukubali kukaimu nafasi hiyo ni sawa na kukubaliana na uamuzi wa kamati ya utendaji ya kumsimamisha Katibu huyo katika kipindi hiki ambacho chama kinaelekea kwenye uchanguzi mdogo wa udiwani kata ya Namikango, uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchanguzi mkuu hapo mwakani.
“Leo tunategemea kuingia kwenye chaguzi sio vyema kuondoana bila sababu za msingi “ alisema China.
Mwenyekiti wa wilaya wa Chama hicho, Ahmadi Likolovela alipoulizwa kuhusiana na suala hili alikiri kuwa kamati ya utendaji imemsimamisha katibu huyo kwa madai ya kusababisha
kukivuruga na kukihujumu chama kwa kushiriki katika kusambaza na kusainisha waraka wa kughushi ambao una lengo la kutaka kukivuruga chama.
“Ni kweli kamati ya utendaji ilikutana na kujadiliana kuhusiana na mwenendo wa Katibu wetu na kufikia uamuzi wa kumsimamisha mpaka pale utakapotolewa uamuzi mwingine au atakapoomba radhi” alisema Likolovela.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.