SIMULIZI | DOKTA SIUMWI HUKO | SEHEMU YA PILI

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
SEHEMU:  YA PILI 

MTUNZI: SKNL BRAND
MAWASILIANO: 0673299988

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
ILIPOISHIA
"Kwa hiyo tatizo kubwa ni Mtoto tu anti yangu?"
"Ni mtoto tu."
"Miraji unamjua?"
"Ndiyo, ni rafiki wa mume wangu Masofa kwani vipi dokta, mbona umemtaja huyo?"

ENDELEA NAYO MWENYEWE......
"Ah! Nimeangalia kwenye maelezo yako, nikagundua kuwa mnatoka eneo moja kwa maana ya ubalozi" Dokta Kisarawe alijibu huku akimuangalia Sulee kwa macho ya kumkagua f'lani hivi.

"Ooh!, maana nilishangaa ni kwa nini umuulize huyo na umejuaje kama ninafahamiana naye," Sulee alihoji huku akiyakimbiza macho yake pembeni baada ya kukutanisha na ya Dokta Kisarawe.

"Hata mkewe alikuwa na tatizo kama la kwako, lakini aliponea kupitia mikono hiihii"
"Kweli dokta?"
"Kweli nakuambia, niamini mimi."
"Mm!, sawa lakini nimesumbuka sana kwani naumia kukosa mtoto jamani" alisema Sulee safari hii akionesha sura ya upole zaidi, hali iliyomfanya Dokta Kisarawe amkazie macho zaidi.

"Kwani mmehangaika kwa muda mrefu sana anti?"
"Yaani wee acha tu dokta, ikishindikana na hapa itabidi niridhike tu kuwa sikupangiwa kuzaa kabisa"

"Ndoa yenu ina muda gani sasa?," Dokta Kisarawe alizidi kumdadisi Sulee huku muda nao ukizidi kuyoyoma na tayari saa iliyokuwa ukutani ilisomeka saa mbili na dakika nne.

"Miaka mitatu sasa dokta"
"Mm..!"
"Mbona unaguna dokta jamani, au huamini?"

ITAENDELEA......!!!!

*********

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post