MOHAMED MATUMLA AMCHAPA NASSIBU RAMADHANI NA KUIBUKA NA BODA BODA

clip_image001Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akimwadhibu Bondia Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa raundi kumi uliofanyika usiku wa sikukuu ya krismas na kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9. Matumla alishinda kwa pointi mpambano huo na kuibuka na bodaboda hiyo.

Bondia Mohamed Matumla (kushoto) akipambana na Bondia Nassibu Ramadhani wakati wa mpambano wao wa kugombania pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni 1.9.

Kwa upande wa Masumbwi ya kina Dada,Bondia Lulu Kayage (kushoto) akipambana na Bondia mwenzake Mariam Abdallah wakati wa mpambano wao wa kusherehekea sikukuu ya krismas.Bondia Lulu Kayage alishinda kwa KO.

Bondia Hamis Ajari (kushoto) akipambana na Cosmas Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika wakati wa sikukuu ya krismas.Cheka alishinda kwa point.

Baadhi ya mashabiki waliouhulia mpambano huo uliokuwa mkali na wakuvutia.

Picha na Super D Blog.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post