Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC)
Kenneth Simbaya akimkabidhi vyeti maalum mmoja kati ya viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari nchini ,vyeti ambavyo vitaanza
kutolewa kwa wanachama wa vilabu ambao wamepatiwa mafunzo mbali mbali.
Na Abdulaziz Video,Mwanza
WANAHABARI nchini wametakiwa kujenga umoja katika kupinga sheria kandamizi ya vyombo vya habari na wanahabari nchini inayatarajia kupitishwa na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Meneja wa uthibiti wa ubora kutoka baraza la habari Tanzania (MCT)
Pili Mtambalike ametoa kauli hiyo leo jijini Mwanza wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya kishujaa na uandishi uliotukuka ya Daudi Mwangosi .
Mtambalike amesema kuwa idadi ya waandishi kutekwa na kuuwawa
imezidi kuongezeka hapa nchini huku kasi ya serikali kuvifungia
vyombo vya habari pia inaendelea kuongezeka .
Hivyo iwapo wanahabari nchini hawataungana katika kupinga
manyanyaso dhidi ya vyombo vya habari na kupinga sheria
kandamizi dhidi ya vyombo vya habari na wanahabari suala la uhuru
wa vyombo vya habari nchini litaendelea kubaki ndoto.
Kwa upande wake rais wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari
Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya alisema kuwa tuzo hiyo inayotolewa
ni tuzo ya kwanza kutolewa nchini Tanzania kwa waandishi wanaopata matatizo wakati wanatekeleza wajibu wao.
Simbaya alisema kuwa UTPC imeamua kuanzisha tuzo hiyo kama njia
ya kuwapa moyo wanahabari na kuuthibitishia umma kuwa wanahabari nchini hawatakata tamaa katika kutumikia tasnia hiyo.
Alisema iwapo jamii inapaswa kujua ni vema serikali kukubali kutoa habari kwa jamii inayopasa kujua na inayo haki ya kupata habari.
“ Serikali itambue kuwa inapohitaji wananchi kuchangia maendeleo ni vema itambue kuwa wananchi hao wana haki ya kupata taarifa mbali mbali ya kile walichochangia, ndani ya tukio la mauwaji ya Mwangosi tumejifunza mambo mengi sana kwani tunapofanya kazi zetu wapo wasiopenda kuona tunafanya kazi zetu hiyo”
Pia alisema ni vizuri wananchi kutambua kuwa wakati wanahabari
nchini wakitetea kupata habari wasifikiri wanahabari
wanajipigania wao .
Kwani alisema kuwa jitihada za wanahabari kupigania uhuru wa
kupata habari zinapaswa kuungwa mkono na kila raia wa Tanzania
ambayo ana haki ya kupata habari.
Jaji mkuu tuzo hiyo Hamza Kasongo alisema kuwa mchakato wa kumpata mshindi ulifanyika kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia septemba hadi Octoba mwaka huu.
Tuzo hiyo ya uandishi wa habari wa kishujaa na utumishi
uliotukuka ya Daudi Mwangosi imetolewa kwa Absalom Kibanda mahariri wa kampuni ya new habari (2006) Ltd na mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini (TEF).