UTPC YAANZA UTARATIBU WA KUTOA VYETI KWA WANACHAMA WA VILABU WANAOPEWA MAFUNZO MBALI MBALI

DU7A0346Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC)
Kenneth Simbaya akimkabidhi vyeti maalum mmoja kati ya viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari nchini ,vyeti ambavyo vitaanza
kutolewa kwa wanachama wa vilabu ambao wamepatiwa mafunzo mbali mbali.
DU7A0354UMOJA wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeanza
utaratibu wa kutoa vyeti maalum kwa wanachama wa klabu za
waandishi wa habari nchini ambao wanapatiwa mafunzo mbali mbali.

Na Abdulaziz Video,Mwanza
Mkurugenzi mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan alisema kuwa vyeti
hivyo vimeanza kutolewa baada ya maadhimio ya wajumbe wa mkutano mkuu .

Hivyo alisema kuanzia sasa wanachama wa vilabu ambao watapewa
mafunzo wanachama wake watapewa vyeti maalum .

Pia alisema vyeti hivyo vitakuwa vya viwango vya juu na vinaanza
kutolewa sasa kwa vilabu hivyo.

Wakati huo huo umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania
(UTPC) umewataka viongozi wa vilabu hivyo mikoani kutumia
changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao kujipanga badala ya
kuzichukia changamoto hizo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mwanza na Rais wa UTPC Kenneth
Simbaya wakati akifungua mkutano mkuu wa wanachama wa klabu za waandishi wa habari .

Simbaya alisema kuwa mbali ya kuwepo kwa mafanikio makubwa katika klabu vya waandishi wa habari nchini ila bado wapo baadhi ya
viongozi ambao wameendelea kukwepa changamoto mbali mbali badala ya kuzifanyia kazi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post