Timu ya Soka Taifa ya Wanawake ya Tanzanite, imeibugiza tena timu ya wanawake ya Msumbiji j mabao 5 -1. katika mchezo wa marudiano uliofanyika leo nchini Msumbiji.
Mabao hayo ya ushindi ya Tanzanite yalifungwa na Selda Boniface amefunga mabao matatu, Vumilia Maarifa bao moja na Dionisia Athanas bao moja. Timu hiyo ya Msumbiji imetolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 15-1.
Tanzanite wanasubiri mshindi wa mechi kati ya Afrika kusin na Botswana ambapo wakishinda wataingia rasmi kwenye michuano hiyo ya kuwania Kombe la Dunia
Tags
SPORTS NEWS