TAJI LA MISS UNIVERSE 2013 LAENDA KWA VENEZUELA

clip_image001Mlimbwende Gabriela Isler, ambaye ni Miss Universe Venezuela 2013, anavishwa taji na  Olivia Culpo, Miss Universe 2012, kwenye fainali za Miss Universe katika ukumbi wa  Crocus City Hall jijini Moscow, Russia, usiku wa kuamkia leo. Kwa ushindi huo Venezuelan imeshashinda mataji 7 ya Miss Universe, 6 ya Miss World, 6 Miss International na 1 la Miss Earth.

clip_image002Bongo bado tupo tupo kwanza, ingawa mwakilishi wetu Betty Boniface kajitahidi sana kwa mavazi ya nyumbani na pozi za kimataifa kama inavyoonesha hapo chini. Iko siku na sisi tutakenua tu...

clip_image002[12]Betty alitinga na mavazi ya Tingatinga mkeka wa ukindu na

clip_image002[14]Vazi la Batik na urembo wa Kimasai vilimtoa vilivyo. Ila basi tu...

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post