Wanafunzi zaidi ya saba wa kidato cha kwanza na tatu mwaka 2013 katika shule ya sekondari Kiangara wilayani Liwale mkoani Lindi wamekatisha masomo baada ya kupata ujauzito mimba na kuozeshwa.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi na wananchi wa kijiji cha Kiangara wilayani Liwale wakati walipokuwa wanazungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea kijiji hapo jana.
Akizungumza kwa uchungu na uzuni kubwa mkazi wa kijiji hicho Abdala Mbenu alisema tatizo la utoro na mimba katika shule ya sekondari ya kata kiangara limekuwa kikwanzo katika maendeleo ya elimu kwani hadi sasa zaidi ya wanafunzi watano wamekatisha masomo kwa kupewa ujauzito.
Mbenu alisema kuwa pamoja na tatizo hilo changamoto kubwa kutoa
ushirikano katika kuwa taja wanao husika na mimba hizo kwa kuhofia
kukosa fedha za rushwa watakazo mtoza muhusika kwa kufanya kitendo hicho.
Aliongeza kuwa pia wanafunzi wenyewe wamekuwa wakidanganya kwa kuwataja wahusika kwa majina yasiyotambulika katika eneo hilo na wakati mwingine hudai kuwa wahusika wamekufa kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.
Kwa upande mtendaji wa kijiji cha Litou Mfaume Petya alisema serikali
ya hicho inashindwa kuwachukulia hatua watu wanaofanya vitendo hivyo kutokana na wazazi na wanafunzi wenyewe kushindwa kutoa ushirikiano na serikali.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.