Unknown Unknown Author
Title: EXCLUSIVE KUTOKA KWA ALI KIBA: "NI WAKATI WANGU WA KUAMKA KATIKA USINGIZII ULIYOJAA MAUMIVU NA DRAMA"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hitmaker wa Cinderela na Dushelele, Ali Kiba ambaye leo anasherehekea birthday yake ya kutimiza umri wa miaka 27, amefunguka kwa kusema alik...

clip_image002Hitmaker wa Cinderela na Dushelele, Ali Kiba ambaye leo anasherehekea birthday yake ya kutimiza umri wa miaka 27, amefunguka kwa kusema alikuwa kimya kutokana maisha ya muziki anayosema yamejaa drama, mateso na mambo mengi.

Akizungumza na Bongo5 leo, Ali Kiba amesema muziki wa Tanzania umejaa drama zilizomfanya atulie kidogo kutafakari na ili kusudi ajue jinsi ya kukabiliana na changamoto zake.

“Nashukuru Mungu nimetiza miaka 27, ni wakati wangu wa kuamka katika usingizi uliyojaa maumivu,drama na mambo mengi ambayo yameweza kunikalisha kimya. Sitaki kusema moja kwa moja kwamba nilikuwa kimya kwasababu maalum ambayo hata ingemkuta mwingine lazima angetulia,” Ali Kiba ameiambia Bongo5.

“Namalizia audio na video ambavo ni kali sana. Unajua nimekuwa nikipokea maoni mengi kwenye Twitter, Instagram na baadhi ya rafiki zangu wakinitaka niamke nifanye mambo. Kwahiyo nadhani muda wangu umefika wa kuamka na kufanya yale mambo ambayo nilikuwa nayafanya. Huu ni muda wa kutoka kutoka nilipokuwa.”

Happy Birthday Ali K and welcome back.

Credit-BONGO5.COM

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top