Hatimaye Shimo lazibwa jana na Kampuni ya simu Tanzania.....
Na Abdulaziz, Lindi
Mtandao huu ulilipoti shimo lililokuwa katika eneo la soko kuu Mjini Lindi kuwa ni kero kwa watumiaji wa Barabara hiyo kwani huwa inaleta ajali mbalimbali hatimae shimo hilo limezibwa jana na Kampuni ya simu Tanzania. (Kama hukusoma bofya hapa)Chakusikitisha nilipoenda leo kupiga picha shimo likiwa limezibwa baadhi ya Vijana walinifukiza na kuropoka kuwa Picha zangu zimezuia ulaji wao kwa kuwa ni magari mengi na bajaj zilikuwa zikitumbukia na wao kufaidika kwa kupata chochote kitu siku zinaenda......
Je tutafika kweli? na Je tuache kufichua kwa ajili ya maendeleo ya Jamii yetu? Hebu Tuambie mdau wetu
Tags
HABARI ZA KITAIFA