Wachezaji wakiingia uwanjani ilikuendelea na Mechi iliyochezwa siku ya Jumamosi uwanja wa Ilulu katika Bonanza la Paris Club
Benchi la Ufundi la Timu ya Mashabiki wa Simba walioibuka washindi katika Mechi hiyo
Paris Club, Club ya Burudani ndani ya Lindi imetimiza mwaka mmoja wa Burudani ndani ya Manispaa ya Lindi. katika kusherehekea siku hiyo Club hiyo imewaalika wadau wake wote wa mji huu kushiriki katika michezo mbali mbali ikiwa ni kukimbiza kuku na kuvuta kamba pamoja na michezo ya mpira, ikiiwa ni kwa upande wa wasichana na wavulana hao wote wakiwa katika makundi mawili nayo ni mashabiki wa Simba na Yanga.
Wachezaji wa Timu ya Mashabiki wa Yanga wakisubiri uamuzi wa Waendesha mashindano kuongezwa dakika au kupigwa penalt baada ya kutoak suruhu 2 – 2.
Mashabiki wa Yanga kwa upande wa wanawake waliibuka mabingwa katika mchezo wa netball, kwa upande wa wanaume washabiki wa Simba walitawazwa mabingwa kwa sababu Mashabiki wa timu ya Yanga Kugomea kuendelea kucheza dakika za Nyongeza mara baada ya Dakika za Kawaida kuisha na matokeo kuwa Ni Bao 2 – 2.
Mashabiki wa Yanga waligomea mchezo huo wa kuongeza dakika kwa kile kilichosemwa kuwa wamecheza katika jua kali na tayari wamekwisha choka hivyo walitaka zipigwe Penalt tu,
Uongozi wa waendesha mashindano katika Bonanza hilo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Paris Club ndg Saidi Matengula, Salma VaaDude, Segesela.
Lakini Viongozi walioandaa mashindano hayo ilionesha dhahili kuwa walikuwa wapenzi wa timu ya mashabiki wa simba kwakile kilichoonekana kiwanjani hapo kwa kuamrisha ziongezwe dakika thelathini na kuruhusu timi ya Mashabiki wa simba kubadilisha timu nzima na kuingiza wachezaji wapya huku wakijua kuwa timu ya Yanga walikuwa hawana wachezaji wa Akiba na kujua lazima watawafunga kwa jinsi walivyokuwa wamechoka.
Hivyo waliamua kugoma na kutoingia uwanjani na kufanya kupatikana ushindi kwa Timu ya Mashabiki wa Simba.
**********************************************
USIKU ILIKUWA NI BIRTHDAY PARTY NA WATU WALIFURIKA KUSHEREHEKEA PARTY HIYO CHEKI PICHA BAADHI YA MATUKIO
Mgeni rasmi akikuwa ni Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi ambae ni wa tatu kutoka kulia akiwa na mkurugenzi wa Paris Club na wageni waalikwa
Wanakamati wa sherehe wakiwa katika furaha wakati sherehe hiyo ikiendelea katika viwanja vya eneo la club hiyo.
Wadau wakitokelezea na Camera ya Lindi yetu iliyokuwepo eneo hilo, kushoto ni (Husna Shop na Salma VaaDude)
Mc aliyeongoza Sherehe nzima kwa jina ULEDI
Mdau mkubwa wa Paris Club Ndg: Mnonjela nae akiwa na Mkewe alikuwepo kama mgeni mwaalikwa.
Mr and Mrs Said Matengula Mkurugenzi wa Paris Club akiwa na familia yake katika kusherehekea mwaka Mmoja wa Burudani(Paris Club)
Shangpen zilifunguliwa………
Keki ilikatwa pia……..
Mgeni rasmi akilishwa keki na Mrs Paris Club
Mrs Paris Club akiwa mwenye furaha katika sherehe hiyo….
Mdau mkubwa wa Paris Club ndg Hassani Mnyaya akiwa na Mdau mwenzake
Wadau wakiendelea kuburudika na kujiachia na Camera Yetu
Mr VaaDude wakwanza kushoto akiwa na wadau wenzake
Hadija Mkadamu akiwa ndani ya viwanja hivyo tayari kusherehekea Mwaka mmoja wa Burudani ndani ya Viwanja vya Paris club
Wadau wanguvu wakiendelea kusherehekea tafrija hiyo….
Mr and Mrs Sule nao walikuwepo katika kujumuika na ndugu jamaa na marafiki katika usiku huo wa kutimiza mwaka mmoja wa burudani wa Paris Club.
Baadhi ya wafanyakazi wa Paris Club wakiwa katika picha Kutoka kushoto ni Dada Mwana na Dullah Kibajaji
Hakika ilikuwa party ya aina yake kwani hakuachwa mtu katika kula au kunywa hata wale waliojitokeza kwa kutochangia waliburudika vilivyo.
Tyme ya Misosi kama kawa watu walijukuika katika kujipatia milo waitakayo
Wanakamati walioandaa sherehe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja
Usafiri ulikuwepo masaa yote ila duh madereva waliuchapa usingizi kama mmoja wa madereva boda boda aonekanavyo hapo juu katika picha
Picha zote na Kilozo FS