SIMBA SC YAPUNGUZWA KASI NA WATOTO WA MKWASA, AZAM NA COASTAL HAKUNA MBABE

clip_image001Juma Nyosso wa Coastal akimdhibiti John Bocco wa Azam

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo, huku vinara Simba SC wakipunguzwa kasi kwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na

Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 8 kupitia kwa Said Dilunga na likadumu hadi mapumziko.

Simba walisawazisha kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 53 mfungaji akiwa Amissi Tambwe.

Beki George Michael alimsukuma Betram Mwobeki ndani ya eneo la 18, mwamuzi akapuliza filimbi kuadhiria mkwaju huo.

Wachezaji wa Ruvu Shooting walionekana kutokukubaliana naye na ilichukua takribani dakika moja hadi mkwaju huo ulipopigwa kifundi na Mrundi huyo na kujaa wavuni.

Pamoja na mabadiliko kutoka kila upande, mwisho timu hizo hazikuweza kupata mabao ingawa Shooting walipoteza nafasi nyingi za wazi.

Azam pia wakitoka sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post