MAJI YA NDANDA YAFUNGIWA KUZALISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA

clip_image001Kampuni ya Ndanda Pure spring water ya mkoani Mtwara imefungiwa kwa muda usiojulikana.

Hii ni kutokana na kubainika kuwa maji yake yaliyopo sokoni hivi sasa ni machafu.

Akiongea na radio Pride FM ya mjini hapa, afisa afya wa mkoa amesema sampo ya maji hayo imepelekwa Dsm mamlaka ya chakula na dawa ili yafanyiwe uchunguzi kuona kama uchafu huo una athari zipi kwa mlaji na kwamba tayari ameshapeleka barua kwenye kampuni hiyo kusimamisha shughuli za kiwanda hicho.

Source: Amka Na Pride Fm

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post