UCL: PRESHA KWA CHELSEA, DORTMUND

clip_image002UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI ipo kilingeni Jumanne na Jumatano Wiki hii kwa Timu 32 zilizo Makundi 8 ya Timu 4 kila moja kucheza Mechi zao za pili na tayari Chelsea na Borussia Dortmund wako kwenye presha ya kusaka ushindi wao wa kwanza baada ya kufungwa katika Mechi za ufunguzi za Makundi yao.

Vigogo wa Barani Ulaya, Barcelona, Real Madrid, Bayern Munich na Manchester United walianza vyema kwa kuteremsha vipigo na Mechi zao jumla ya Mabao 17 kufungwa lakini Chelsea, Mabingwa wa Ulaya Mwaka 2012, walichapwa Nyumbani Bao 2-1 na FC Basel na Borussia Dortmund, ambao walifungwa kwenye Fainali ya Mwezi Mei Mwaka huu na Mabingwa Bayern Munich, walichapwa pia 2-1 Ugenini na Napoli.

PRESHA KWA CHELSEA, DORTMUND

Msimu uliopita, Chelsea waliweka Historia ya kuwa Bingwa wa kwanza Mtetezi kutolewa Hatua ya Makundi na kutupwa Europa Ligi na safari hii, chini ya Kocha mpya Jose Mourinho mwenye Rekodi nzuri kwenye UCL, walitarajiwa kufanya vyema lakini wameanza vibaya kwa kuchwapwa katika Mechi yao ya kwanza tu.

Jumanne Chelsea wapo Ugenini huko Romania kucheza na Steaua Bucharest ambako Msimu uliokwisha kwenye Europa Ligi walifungwa 1-0.

Dortmund wako Nyumbani kucheza na Marseille na hawana nafasi ya kuteleza tena.

HISTORIA ITAJIRUDIA CELTIC PARK?

Mwezi Novemba Mwaka Jana kwenye UCL, Celtic waliifunga  Barca 2-1 Uwanja wa kwao Celtic Park na Jumanne Celtic wanaikaribisha tena Barca kwenye Mechi ya Kundi H na safari hii Barca hawana Supastaa wao Lionel Messi ambae ni Majeruhi.

Je Historia itajirudia?

MOYES KUPOZWA NA ULAYA?

Manchester United David Moyes huenda akafurahia kucheza Ulaya badala ya England kufuatia Wiki aliyochapwa 4-1 na Mahasimu wao Man City kwenye Ligi, Jumatano kuifunga Liverpool 1-0 na kuitoa kwenye Capital One Cup na kisha Jumamosi kutwangwa bila kutarajiwa 2-1 Nyumbani kwao Old Trafford na West Bromwich Albion Jumamosi kwenye Ligi.

Safari hii wapo kwenye Kundi A la UCL Ugenini huko Ukraine, ambako Klabu za England haziwahi kushinda, kucheza Mechi yao ya pili na Shakhtar Donetsk baada kushinda Old Trafford Mechi ya kwanza kwa kuichapa 4-2 Bayer Leverkusen.

Tayari Moyes amekiri nafasi yao ya Ubingwa Ulaya ni finyu kwa sababu Timu yake inawakosa Wachezaji watano au sita wa kiwango cha Dunia.

Huenda hii ni plani tu ya kujiondolea presha au lawama ikiwa hawafanyi vyema.

BIGI MECHI YA RAUNDI HII - MAN CITY V BAYERN MUNICH

Ni Kundi D na Mechi kati ya Man City na Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich ndio Bigi Mechi ya Raundi hii huku kila Timu Msimu huu ikiwa na Meneja mpya, Manuel Pellegrini kwa City na Pep Guardiola kwa Bayern.

Kwa Misimu miwili iliyopita Man City wameshindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UCL lakini safari hii wameanza kwa ushindi mkubwa wa Ugenini walipowachapa at Viktoria Plzen 3-0.

Bayern nao waliwafunga kirahisi CSKA Moscow 3-0.

Wikiendi hii, kwenye Ligi zao, Man City ilichapwa 3-2 na Aston Villa na Bayern kuifunga Wolfsburg 1-0.

MATOKEO-Mechi za Kwanza:

Jumanne 17 Sep 2013

Manchester United FC 4 Bayer 04 Leverkusen 2

Real Sociedad de Fútbol 0 FC Shakhtar Donetsk 2

Galatasaray A.Åž. 1 Real Madrid CF 6

FC København 1 Juventus 1

SL Benfica 2 RSC Anderlecht 0

Olympiacos FC 1 Paris Saint-Germain 4

FC Bayern München 3 PFC CSKA Moscow 0

FC Viktoria Plzeň 0 Manchester City FC 3

+++++++++++++++++++++++++++++

Jumatano 18 Sep 2013

FC Schalke 3 FC Steaua BucureÅŸti 0

Chelsea 1 FC Basel 2

Olympique de Marseille 1 Arsenal 2

SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1

FK Austria Wien 0 FC Porto 1

Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1

AC Milan 2 Celtic FC 0

FC Barcelona 4 AFC Ajax 0

[Zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku]

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post