NINI KINAJIRI?? KULIKONI OLD TRAFFORD??
JUMAMOSI iliyopita, Old Trafford ilishuhudia West Bromwich Albion ikiifunga 2-1 Manchester United kwa mara ya kwanza Uwanjani hapo tokea Mwaka 1978 na kuwatupa Mabingwa hao wa England Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England.
================================
TAKWIMU
-Manchester United wapo Nafasi ya 12 kwenye Ligi.
-Wamefungwa Mechi 3 kati ya 6 za Ligi walizocheza.
-Huu ni mwanzo mbovu kwa Miaka 24 tangu Mwaka 1989/90, Sir Alex Ferguson alipoiongoza Timu na kuambua Pointi 7 katika Mechi 6 kama ilivyo sasa.
================================
Mara ya mwisho kwa Man United kujikuta wako Nafasi ya 12 au chini yake baada ya Mechi 6 ni Mwaka 1986 ambapo Meneja alikuwa Ron Atkinson na Man United walikuwa Nafasi ya 19.
Klabu ikamwita Mtu aitwae Alex kuja kuinusuru.
Sir Alex Ferguson alitua Manchester United Novemba 1986 na, kama wanavyosema, yote yaliyojiri baada ya hapo ni Historia kubwa.
Huu ni Mjadala mzito huko England na kwingineko kwenye Anga za Soka Duniani na baadhi ya mambo yanayotajwa kama sababu za kudorora Manchester United hivi sasa ni kama ifuatavyo.
Ugumu wa Uhamisho na hasa kupata Viungo wapya na bora
Mara baada ya kufungwa na WBA Jumamosi iliyopita, David Moyes, Meneja mpya wa Man United, alikiri Timu kukosa Watu wenye cheche ya kuiongoza Timu.
Hili hasa limehusishwa na kukosa Viungo imara, hasa baada kustaafu Paul Scholes, wa kuibeba Timu hasa wakati mbovu kwenye Mechi.
WBA walidhihirisha kupwaya kwa idara ya Kiungo ya Man United huku Mchezaji wao Stephane Sessegnon akitamba kwa kuongoza ‘Kaunta Ataki’ nyingi na kuleta balaa kwa Michael Carrick huku Anderson akionekana legelege hapo katikati.
Kabla Mechi hiyo, Jumapili iliyopita, Carrick na Marouane Fellaini, walizidiwa kila kitu walipokutana na Kiungo ya Man City ya Yaya Toure, Fernandinho, Samir Nasri na Navas na kuchapwa 4-1 lakini waliimarika kidogo kwenye Mechi hiyo alipoingizwa Tom Cleverley na kucheza vizuri na hata kupata Bao lao moja.
Man United walijaribu kununua Viungo kabla Msimu huu kuanza lakini waliwakosa walengwa wao kina Cesc Fabregas, Luka Modric na Anders Herrera.
Meneja
Tofauti kubwa ya Msimu uliopita na huu ni Sir Alex Ferguson.
Yeye ndio Meneja mwenye mafanikio makubwa sana katika Historia ya Soka ya Uingereza.
Wapo walioanza kumsakama Moyes lakini ni mapema mno kwako kuingia kwenye Ofisi aliyowahi kukaa Sir Alex Ferguson na kutegemea mabadiliko na mafanikio ya ghafla.
Hata Ferguson mwenyewe alietua Old Trafford Novemba 1986 alitwaa Kombe la kwanza, FA CUP, Msimu wa 1989/90 na Ubingwa wake wa kwanza kwenye Msimu wa 1992/93.
Wachezaji wanabidi wawajibike
Ukimwondoa Wayne Rooney, ambae alikumbwa na sakata la kutaka kuhama mwanzoni mwa Msimu huu, hakuna Mchezaji yeyote anaejituma na kujitutumua kusaka ushindi kwa udi na uvumba.
Kukosekana kwa Robin van Persie Wiki iliyopita kutokana na maumivu kulichangia mno ubutu wa Timu lakini kupwaya kwa Wakongwe Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Michael Carrick ndiko kumeleta wasiwasi mkubwa.
Ferdinand, sasa Miaka 35, ndie alikuwa uchochoro kwenye Mechi walizofungwa na Liverpool huko Anfield na kusababisha Daniel Sturridge afunge Bao pekee na huko Etihad Sergio Aguero na Alvaro Negredo walimzunguka vilivyo.
Jumamosi, kwenye Mechi na WBA, ambayo Vidic hakucheza, Ferdinand alishindwa kumdhibiti Victor Anichebe na pia kudanganywa kirahisi na Morgan Amalfitano aliefunga Bao la kwanza kirahisi mno.
Kwenye Winga, Wachezaji Antonio Valencia, Ashley Young na Shinji Kagawa wamepwaya mno.
Dhidi ya Man City, uchezaji wa Ashley Young ulitia uchungu.
Kubaki kumtegemea Ryan Giggs, Mchezaji anaekaribia Miaka 40, ni hali ya kusikitisha na kutisha.
Moyes anazidisha ubovu kwa kubadili Timu kila Mechi na kuingiza Wachezaji wasiostahili wakati wa Mechi
Ni kweli kuna tofauti kubwa ya kusimamia Kikosi cha Wachezaji 16 tu wa Timu ya Kwanza huko Everton na kutua Manchester United ambako Kikosi cha Kwanza kina Wachezaji 25 na wote ni Wachezaji wa Kimataifa wanaochezea Nchi zao.
Na hayo ndio mabadiliko aliyoyakuta David Moyes kutoka Everton kwenda Man United.
Ni wazi Moyes alifanya makosa mwanzoni tu mwa Msimu huu na hasa uamuzi wake kuwachezesha pamoja Rio Ferdinand na Nemanja Vidic mara 3 ndani ya Wiki moja, dhidi ya Crystal Palace, Bayer Leverkusen na Manchester City.
Hawa hawajacheza pamoja Mechi 3 ndani ya Siku 8 tangu Mwaka 2010 na baada kuwa ubwete walipocheza na Man City haiwezekana tena kwa Moyes kurudia kosa hilo.
Kinachotakiwa kufanywa na Moyes ni kupanga Timu yake kwa kuangalia Mechi zipi zitawakabili mbele yao.
Kwa hilo, Sir Alex Ferguson, alikuwa ni fundi mkuu.
Mara nyingi Sir Alex alikuwa akiongelea kuwa alikuwa anakijua Kikosi chake cha Mechi yao ya Wiki mbili baadae na alihakikisha Wachezaji wake wanabaki na motisha licha ya kupigwa Benchi kwa kuwahakikishia kucheza Mechi fulani ya baadae.
Jordi Cruyff, Mtoto wa Nguli wa Holland Johan Cruyf, aliewahi kuichezea Man United kati ya Mwaka 1996 na 2000, amewahi kueleza: “Sir Alex alikuwa na hisia kubwa za kuwamudu Watu. Nilishangazwa sana na yeye hasa pale kama Meneja anakuja kwako na kukwambia: ‘Huchezi leo, lakini tulia, fanya mazoezi vizuri kwa sababu nakuhitaji kwa Mechi kubwa baada ya Wiki mbili.’ Mie niliwahi kumuuliza sasa ikiwa kila Mtu atafunga Hetitriki utanichezeshaji? Lakini yeye alinijibu: ‘Hilo ni tatizo langu usiwe na wasiwasi!’
Kwa hili, pengine Moyes anastahili kusamehewa kwani alikabiliwa na Ratiba ngumu yenye Mechi kubwa na ngumu katika muda mfupi.
Lakini Wataalam wamenyooshea kidole upangaji wake wa Timu wenye kasoro kubwa katika Mechi dhidi ya Manchester City na West Brom.
Man United walihitaji nguvukazi kubwa ya kukabiliana na Kiungo ngangali cha Man City na walionekana kuweza kudhibiti idara hiyo pale tu alipoingizwa Tom Cleverley lakini wakati huo walikuwa tayari wameshapigwa Bao 4.
Dhidi ya West Brom, Alex Buttner na Anderson walichaguliwa kucheza lakini wote walipwaya mbele ya Yacob na Mulumbu.
Uamuzi wa kumtoa Shinji Kagawa wakati wa Haftaimu unaonyesha kutokuwa na maamuzi sahihi na ingawa aliingizwa Adnan Januzaj, Mbelgiji wa Miaka 18, aliecheza vizuri kiasi lakini ni kosa lake yeye ndio lilisababisha Bao pale pasi yake mbovu iliponaswa.
Iko wapi ile ari ya kupigana Kufa na Kupona hadi Filimbi ya Mwisho iliyokuwepo chini ya Sir Alex Ferguson??
Waliposawazisha Bao walipocheza na West Brom kwa Bao la Wayne Rooney na wakati huo huo Robin van Persie kuinuka kutoka Benchi la Akiba na kuingia kucheza, hakuna hata Mtu mmoja alietegemea West Brom watashinda.
Lakini Man United walishindwa kuja juu na kufifia na ni WBA ndio waliofunga Bao la Pili na kushinda Mechi 2-1.
Na hilo ndio lilitokea Kipindi cha Pili walipofungwa na Man City, na lilijionyesha walipotoka Droo na Chelsea Uwanjani Old Trafford ambako Man United ya nyuma ingeweza kuongeza presha na kushinda na huko Anfield wangeweza pia hata kupata Sare.
Katika Mechi na WBA, walipokuwa nyuma Bao 2-1, kila Mtu Old Trafford alitegemea Man United itasonga mbele, kuibana WBA na kuleta kizaazaa cha kusawazisha na kushinda lakini badala yake walififia na kupotea kabisa.
Inasemekana Sir Alex Ferguson alikuwa akiifundisha Timu yake kucheza Dakika 15 za mwisho za Mechi ili wahakikishe wapo tayari kugeuza kipigo kuwa Sare na Sare kuwa Pointi 3.
Chini ya Moyes hilo halijaonekana hadi sasa.
Nini kitajiri??
Kuwa Pointi 8 nyuma ya Kinara wa Ligi baada Mechi 6 si tatizo kubwa kwa sasa lakini matokeo mazuri yanatakiwa kuanzia sasa kwani kutotwaa Ubingwa si maafa ila maafa ni kutomaliza kwenye 4 Bora na hivyo kutofuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Na maafa makubwa mno ni hilo kutokea kwa Kikosi hicho hicho ambacho ndio kilitwaa Ubingwa.
MOYES==KIMBEMBE KINACHOMNGOJA
SOURCE: SOKA IN BONGO

| OKTOBA | SAA | SIKU | |
| UCL | Shaktar Donetsk v Man United | 19:45 | Jumatano Oktoba 2 |
| BPL | Sunderland v Man United | 17:30 | Jumamosi Oktoba 5 |
| BPL | Man United v Southampton | 15:00 | Jumamosi Oktoba 19 |
| UCL | Man United v Real Sociedad | 19:45 | Jumatano Oktoba 23 |
| BPL | Man United v Stoke | 15:00 | Jumamosi Oktoba 26 |
| COC | Man United v Norwich City | Wiki kuanzia Okt 28 | |
| NOVEMBA | |||
| BPL | Fulham v Man United | 15:00 | Jumamosi Novemba 2 |
| UCL | Real Sociedad v Man United | 19:45 | Jumanne Novemba 5 |
| BPL | Man United v Arsenal | 16:10 | Jumapili Novemba 10 |
| BPL | Cardiff v Man United | 16:00 | Jumapili Novemba 24 |
| UCL | Bayer Leverkusen v Man United | 19:45 | Jumatano Novemba 27 |
| BPL=LIGI KUU ENGLAND | |||
| UCL=UEFA CHAMPIONZ LIGI | |||
| COC=CAPITAL ONE CUP | |||
SOURCE: SOKA IN BONGO