DK SHEIN AMPONGEZA RAIS WA CHINA

clip_image002Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais wa China, Xi Jinping kwa kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa nchi hiyo.

Katika salamu zake hizo, Rais wa Zanzibar amesema wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa China katika kusherehekea miaka 64 ya uhuru wa nchi hiyo pamoja na urafiki na mshikamano uliodumu kwa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili.

Dk Shein ameitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya China kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika sekta zote za maendeleo chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti.

Ameelezea matumaini yake kuwa ushirikiano baina ya Serikali ya China na Wananchi wa Zanzibar utaendelea kuimarika zaidi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post