Mashoga na Wasagaji wamefunga ndoa iliyoshuhudiwa na mamia ya watu katika Kisiwa cha Rhodes Island na Minnesota jana nchini Marekani.
Ripoti mbalimbali Agosti Mosi mwaka huu nchini Marekani, zinasema kuwa kwa sasa nchini Marekani zaidi ya robo ya Wamarekani wanaunga mkono ndoa za jinsia moja na makanisa mbalimbali yameingia na kuendelea kufungisha ndoa za aina hiyo.
Usiku wa kuamkia leo (kwa saa za Afrika Mashariki) katika Jimbo la Minnesota kumelipuka nderemo na vifijo pale mashoga Zachary Marcus na Gary McDowell walipobadilisha hati za viapo katika ukumbi wa Jiji wa Providence (Providence City Hall) mbele ya Meya wa Jiji hilo Angel Taveras.
McDowell (28) mtafiti katika Harvard Medical School aliyezaliwa Northern Ireland na kwa mujibu wa sheria za taifa hizo kwa sasa zinampa haki ya kuweza kuishi na kuwa na makazi ya kudumu na mumewe.
Marcus (25) ambaye ni Mwanafunzi wa Brown University akinukuriwa na vyombo vya habari nchinihumo amesema imekuwa siku ya furaha kwake na ushindi wa kisiasa.
Majimbo 13 nchini Marekani likiwemo la Wshington ndoa za jinsia maoja zinakubalika bila pingamizi lolote.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kundi la Haki za Mashoga na Wasagaji imesema 30% ya wakazi waliopo nchini Marekani sasa wanaishi katika maeneo ambayo ndoa za mashoga na wasagaji ni haki ya msingi.
Watu akali ya 1,000 hapo jana katika Jiji la Minneapolis (Minnesota) walikusanyika katika ukumbi wa mikutano wakisherehekea ndoa ya 46 ya watu wenye jinsi moja ikifungwa na kupewa Baraka zote na Meya R.T. Rybak.
Gavana wa Jimbo la Minnesota Mark Dayton ametangaza Agosti Mosi kuwa “Freedom to Marry Day” jimbo humo.
Mawakili wamesema Sherehe za mjini humo, zilikuwa za kufana kutokana na ukweli kwamba majimbo yaliyo karibu nayo yamekubali ndoa za jinsia moja.
Gavana wa Chama cha Democrats, Lincoln Chafee ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza kabisa kushabikia ndoa za jinsia moja kisheria, alipokuwa Seneta wa Chama cha Republican anapanga kuhudhuria kikao cha watunga sheria za ndoa za jinsia moja.
Pia jana hiyo hiyo Cathy ten Broeke na Margaret Miles nao wamefunga pingu za maisha wakiwa ni wasagaji wa kwanza kabisa kufunga ndoa katika Providence City Hall.
Watunga sheria waliopo katika Rhode Island chenye waumini wengi wa kikatoliki wamepigana kufa au kupona kwa miaka 16 sasa hata kupitishwa kwa sheria za Mashoga na wasagaji.WAKAZI WA MINNESOTA WAKIUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA AGOSTI MOSI