CARDIFF CITY YAICHAPA MAN CITY BAO 3 - 2

clip_image002 
Freizer Campbell akishangilia goli na wenzake, afunga holi mbili dhidi ya Man City
Cardiff City walicheza kiume na kuwatwanga Manchester City Bao 3-2 na kutwaa ushindi wao wa kwanza katika Ligi Kuu England.
Cardiff City waliisimamisha Man City na Gemu kuwa 0-0 hadi Mapumziko na Kipindi cha Pili Edin Dzeko, katika Dakika ya 52, aliwapa Man City Bao la kuongoza lakini Cardiff wakasawazisha baada ya Shuti la Fraizer Campbell kutemwa na Kipa Joe Hart na Aron Gunnarsson kumalizia wavuni.
Ndipo zikaja Dakika 8 za Mchezaji zamani wa Timu ya Vijana wa Manchester United, Fraizer Campbell, kufunga Bao mbili kwa kichwa na kuifanya Cardiff iwe mbele kwa Bao 3-1.clip_image002[5]Alvaro Negredo aliipa Man City Bao la pili ndani ya Dakika 6 za Nyongeza na kuleta mshikemshike lakini Cardiff walisima imara kulinda ushindi wao wa Bao 3-2.
VIKOSI:
Cardiff: Marshall, Connolly, Caulker, Turner, Taylor, Medel, Gunnarsson, Bellamy, Kim, Whittingham, Campbell
Akiba: Hudson, Cornelius, Noone, Mutch, Cowie, Maynard, Lewis.
Man City: Hart, Zabaleta, Javi Garcia, Lescott, Clichy, Fernandinho, Toure, Jesus Navas, Aguero, Silva, Dzeko
Akiba: Milner, Kolarov, Rodwell, Pantilimon, Nastasic, Negredo, Nasri.
Refa: Lee Probert
TOTTENHAM 1 SWANSEA 0clip_image002[7]
SOLDADO AENDELEA KUIPA USHINDI SPURS!!
PENATI ya Dakika ya 58 iliyopigwa na kufungwa na Roberto Soldado, likiwa ni Goli lake la 4 kwa Mechi 3 katika Timu yake mpya, leo limewapa ushindi wa Bao 1-0 Tottenham waliokuwa wakicheza Nyumbani White Hart Lane dhidi ya Swansea City katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Jonjo Shelvey kumchezea rafu Andros Townsend.
Huu ni ushindi wa pili kwenye Ligi kwa Tottenham kufuatia kuifunga Cardiff City Bao 1-0 katika Mechi ya kwanza na hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Swansea baada ya kuchapwa Bao 4-1 na Man United katika Mechi ya ufunguzi.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Rose, Paulinho, Capoue, Townsend, Dembele, Chadli, Soldado
Akiba: Kaboul, Naughton, Defoe, Friedel, Sandro, Sigurdsson, Carroll.
Swansea: Vorm, Rangel, Chico, Williams, Ben Davies, Shelvey, Canas, Hernandez, de Guzman, Routledge, Michu
Akiba: Amat, Britton, Bony, Lamah, Pozuelo, Tremmel, Richards.
Refa: Neil Swarbrick


















Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post