Sehemu: 9
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: +255 713 133 633
Ilipoishia…
..Nikajikuta mwili wangu ukinisisimka. Nikatamani sana na mimi nimalize kulala na maiti zote haraka nipelekwe kuolewa na rais. Nikafikiria jinsi rais alivyokuwa na nyadhifa kubwa serikalini. Akili yangu ikamfikiria mke wake kwa jinsi nitakavyokuwa simpendi namfanyia vituko. Nikaahidiana na moyo wangu, akili ikakiri kumpa mapenzi ya dhati mpaka awe ananipenda mimi nakumuacha mke wake wa duniani.
“Lakini mama sijaelewa vizuri. Kwani rais mwenyewe ni yule wa duniani?”
Songa nayo sasa….
Wakaangaliana tena uku wakitoa meno yao makali. Meno ya kichawi kisha wakaniangalia na mimi wakaangua vicheko vya kimbeya.
“Adela?”
“Abee!!”
“Hilo swala la wewe kuolewa na rais gani nakuomba nisikwambie kwani mimi siyo msemaji mkuu wa wachawi ila uko tunapoenda utakutana na Diana na atakwambia kila kitu kuhusiana na rais na hadi jinsi ya kulala naye na kumpa mampenzi.”
“Sawa nimekuelewa mama!”
Ilinibidi nijibu kishingo upande japokuwa moyo wangu haukuliafiki kabisa jibu nililokuwa nimepewa na mama. Jibu la kusubiria mpaka tufike nililiona kuwa refu sana.
Haikutuchukuwa muda tukawa tumeshaingia kwenye msitu mkubwa sana.Tukashuka hadi chini na ungo wetu.
“Adela wewe endelea kutushikia mioyo ivyo ivyo mpaka tutakapofika.”
Aliropoka Sonia mmoja kati ya wale wachawi wenzangu. Wakaanza kusaidiana kuwashusha wale watu ambao walipata ajali na kuwachukua. Watu hao wakiwa ni wanaume tupu ambao walikuwa wamevuliwa nguo zao zote nakubakiwa utupu kama walivyozaliwa.Mikono na miguu yao ilionesha kulegea sana na kuwa na damu damu nyingi. Sonia,Sarah,mama wakisaidiana na Tonny wakawa wanawabeba wale watu mgongoni nakuwashusha nje ya gari letu (Ungo). Walipomaliza kuwashusha wote wakawalaza chini kwa mstari mmoja. Wakachuma majani ya miti na kulaza chini kisha wakatumia miguu yao kukanyaga ile miili ya watu maeneo ya midomoni mwao mpaka ikawa nyang’anyang’a na baada ya hapo wakawadumbukizia majani ya miti.Muda wote nilikuwa pembeni nimeibebelea mioyo kifuani mwangu uku mkia na kibuyu vikiwa vimening’inia pembeni ya kiuno changu kwa kutumia kamba ya hirizi.Tonny akayeyuka ghafla naukuacha vumbi jeupe mithili ya majivu yaliotibuliwa kwa kumwagiwa maji ya moto. Haikuchukuwa muda akarudi eneo lile lile alipoyeyukia. Na kwa sasa alikuwa amerudi na misukule sita.
“Adela?’
Yule mama aliniita kwa sauti ya juu na ya ukali”
“Abee”
“Hapa mwanangu tunaweza kwenda sasa katika kambi yetu na utapata fursa ya kuwaona viongozi wetu pamoja na kupewa ruhusa ya kulala na maiti ishirini na baada ya hapo utapewa baraka zote za kwenda kuolewa na rais”
“Sawa mama!’
Niliitikia kwa furaha ya ajabu. Mtetemo! Mikono ikaing’ang’ania ile mioyo kwa nguvu na kwa hisia ya hali ya juu.Mwili ukaugeukia moyo ndani yake, moyo ukatikisika kwa kuyumba yumba mithili ya mlevi aliyelewa sana nakupotea kwake. Ukatoa tabasamu na kuonesha kicheko kwa mwili. Nikasisimka tena!Macho yakarudi kuangaza mbele kuona walichokuwa wakiendelea kukifanya wakina Sonia.Waliwainua nakuwafunga mikono wale watu ambao tulikuwa tumewachukuwa. Wakawa kama wamebebana kwa jinsi walivyokuwa wamefungwa kwa kamba. Misukule takribani sita ilikuwa katika jitihada za kuhakikisha ile miili ya wale watu inabebwa na wao vizuri. Hawakuwa wakiongea. Kwa kawaida ya wachawi huwa wanapenda sana kutumia misukule kwenye kazi zao nyingi na ngumu ikiwa ndio njia yao nyepesi ya kurahisisha kazi zao. Mara nyingi wachawi huchukuwa wale watu duniani ambao katika familia zao huwa ni wa kwanza ama wa mwisho na tena wale ambao hupendwa sana hapa namaanisha wale watu pekee katika familia zao.Huwageuza kwa kuwapumbaza midomo na akili kisha huwafanya misukule.Hutumia madawa ya kichawi ikiwa ni pamoja na kuwakata ulimi na sehemu ya koromeo inayotoa sauti ili wasiweze kutoa sauti kisha huwachukuwa jumla kwa kuwapaka unga wa ugali mwili mzima lakini watu wa duniani wanakuwa wakijua kuwa ni mfu na hata vifo vya hawa watu huwa ni vya utata ama vya ghafla sana pasipo kuugua. Na wakiwazika wanakuwa wamezika gogo ama mgomba.
Kwa muda huu ile misukule ilikuwa uchi uku sura zao zikiwa zimetapakaa unga na tope tope la kichawi kwa kuwafanya watambulike ni misukule na si wachawi. Bega kwa bega wakawa katika kutusaidia kubeba ile miili ya wale watu iliojaa majani midomoni mwao ambayo ilikuwa imeshafungwa kamba. Tulipanga wote mstari mmoja. Mbele kabisa walikuwa ile misukule wakiibebelea ile miili ya watu na nyuma yake alikuwa yule mama na nyuma kabisa nilikuwapo mimi na kina Sonia,Tonny na Sarah. Walinisaidia kushika mioyo na mimi nikabakia na mioyo mitatu mkononi. Njia nzima ilikuwa ni kimya tu uku tukikatiza pori na mapori. Hofu! Ghafla nikajikuta nipo peke yangu eneo lote. Mbele yangu hakukuwa tena na misukule wala wachawi wenzangu. Mikono ilikuwa imebakiwa na ile moioyo mitatu iliokuwa ikinivujia damu damu kifuani mwangu.
“Soniaaa? Tonny?, Mamaaa?”
Nilijitahidi kutoa sauti yangu na kuwaita wote lakini ndio kwanza kimya kikatanda zaidi.Mauza uza! Upepo mkali tena ule wakuzunguka aina ya kimbunga ndio nikaushuhudia mbele yangu. Woga ukanitanda, nikasogea mpaka kwenye mti uliokuwa pembeni yangu. Nikajibanza! Nikashusha pumzi uku nikiutoa mkono wangu mmoja nakuusogeza mpaka karibu na kiuno changu kwa lengo la kutoa kibuyu na mkia. Tahamaki! Sikuona cha kibuyu wala mkia zaidi ya ile kamba iliokuwa na hirizi ikiendelea kuning’inia katika kiuno changu. Machozi yakaanza kunilenga lenga nikajihisi mwili wangu kudhoofu ghafla kwa woga. Nikazidisha kuhema kwa juu juu uku nikiusikiliza moyo wangu upate jibu kutoka kwa akili na kuamua nifanyaje.Nikiwa katika limbi la mawazo.Nikajikuta nikianza kurudi nilipotoka. Ujasiri! Nikatupa ile mioyo yao pembeni uku akili ikiwa imesha shauriana na akili juu ya kurudia ungo wangu tulipokuwa tumeuacha.
“Simama! Adela simama!”
Sauti kali ya kiume na ya kibabe ikatikisa masikio yangu. Masikio yakatikisika.Macho yangu ya kichawi yakapambaza uku na kule kujua sauti inapotokea. Sikuweza kuona kitu zaidi ya kusikia kishindo cha mtu akitembea. Nikaukumbatia mti mwingine kwa nguvu zote mithili ya mwanamke aliyepotelewa na mpenzi wake kwa muda mrefu akampata. Nikayatoa machozi kwa nguvu na hasira. Machozi yakasalimiana na paji la uso. Uso ukabaki na majonzi kwa msisimko wa machozi moto moto yaliokuwa yakiomba njia katika mwili wangu nakudondoka mpaka chini. Majuto! Nikaanza kujuta kisa cha kunileta mpaka uku. Hasira na uchungu ukanizidia kama mama mjamzito wa mapacha. Nikabaki nikisikilizia ule mshindo. Ule mshindo ukawa unazidi kutoa sauti mara nyingi zaidi. Nikahisi umenikaribia karibu. Mwili ukaanza kulowa kwa manyunyu kutoka juu ya mti.Mvua ya ghafla ikaulowesha mwili wangu. Ukauchakaza nakuutakatisha kwa muda utakavyo. Nguvu zikaanza kuniisha Adela mimi, nikaacha kuung’ang’ania mti nakukaa mpaka chini yake.
“Jamila uko wapi? Sophy niokoeni uku nimekuja kubaya sikutaki mimi!”
Nikatoa sauti ya juu lakini haikusaidia kwani ni kama sauti ilikuwa ikinirudia mwenyewe tena zikifuatana na kuwa sauti nyingi nyingi. Mara kukawa tena kimya. Mvua ile iliokuwa ikinyesha ikakata. Suikusikia sauti ya kishindo tena wala mvua zaidi ya eneo la mbele yangu kuwa na maji mengi yaliotulia. Kwa mbali nikaanza kusikia sauti za watu wakiimba nyimbo moja ya kichawi ambayo nilikuwa nikiipenda sana. Nyimbo ambayo huimbwa na wachawi wanapokuwa wamepata kitoweo. Hisia! Nguvu za ajabu zikauteka mwili wangu, woga ukanipotea na kusahau ghafla kilichokuwa kimenitokea. Nikainuka na kusonga mbele uku zile nyimbo zikinivuta. Nikaanza kufuata uelekeo wa zile nyimbo zilipokuwa zikitokea.Nikaruka ruka ndani ya maji nikitaka kuvuka. Hatua takribani kumi nikajikuta siwezi tena kwenda mbele. Miguu ikawa imetumbukia ndani ya tope zito mpaka eneo la karibu na magoti. Tope likaanza kutoa harufu kali. Wadudu aina ya mbung’o wakatawala juu ya tope uku wakitoa harufu kali. Wakaanza kuushambulia mwili wangu eneo lile niliojkuwa nimekatwa maziwa. Wakaanza kulizngungushia maduara na kisha wakaingia mpka ndani ya mwili wangu nakuanza kuufakamia.
“Adela”
Ile sauti ya kiume ikarudia kuita tena. Sikutaka kuitika kamwe. Ikarudia kuita zaidi ya mara sita. Nikashangaa lile eneo lililokuwepo ndani ya tope likizungukwa na idadi kubwa ya wachawi wenzangu. Wakanizunguka uku wakiimba ile nyimbo ya kichawi niliokuwa nikiipenda uku wengine wakiitikia ‘ineku’ wakimaanisha mgeni mualikwa. Mikononi mwao kila mmoja alionesha kushikilia mienge iliokuwa ikitoa moto mkali kuangaza. Wakawa wakinisogelea karibu zaidi. Wakajitokeza Sonia na Sarah wakiwa wameshikilia mioyo mingi zaidi ya ile niliokuwa nimeitupa. Wakanirushia ile mioyo hadi ndani ya tope. Wale mbung’o waliokuwa wakinishambulia wakaiwahi ile mioyo nakuiteketeza. Ikanyumbulika! Halmashauri ya kichwa changu ikafanya kazi haraka nakujua huenda mimi leo ndo kitoweo chao.
******************
**** Inamaana Adela amegeukwa? Sasa yaonekana ni vita ya kichawi kwa makundi. Nini hatma ya Adela baada ya kuingia katika himaya ya kina Sonia?
***** Vipi kuhusu wakina Jamila na Sophy? Wanajua Adela alipo? Na wakiwa wanajua watafanyaje kumnasua Adela?
**** Simulizi hii ni ya kweli na mambo yaliopo ni ya kweli kwa wachawi hakuna hata kimoja kilichobuniwa. Najua lazima kuna baadhi ya wachawi watakuwa wameiona simulizi hii ama kuambiwa na watu. Ni kwamba Adela ameahidi kuwaumbua wachawi wote na njia zao zinazotumika ili watu wa duniani wajue. Kwa pamoja tunaupinga uchawi.
***** LIKE nyingi zinasaidia kuifanya simulizi hii inoge na kuwa tamu zaidi. Gonga LIKE yako simulizi hii.
Tags
HADITHI NA RIWAYA