Sehemu: 12
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: +255 713 133 633
Ilipoishia…
. “Kweli?”
Sikutaka kabisa kichwa changu kiamini yasemayo na Diana. Nikayafumba macho. Halmashauri yangu ya kichwa ikafanya kazi haraka nakukumbuka kuwa kuna mtu niliambiwa anaitwa Diana ambaye alishawahi kuolewa na Raisi yeye ndiye atakayeniambia kila kitu jinsi ya kufika mpaka kwa Rais. Nilijikuta nikiushukuru moyo kwa uvumilivu ulioonesha nakuniongoza mpaka nilipofika. Zile ndoto zangu za kuolewa na Rais zikawa zimeshakubaliana na akili yangu. Nikainuka nakumkumbatia Diana. Diana akanishika mkono nakuniongoza ndani ya maji kuelekea uko ikulu kwa ajili ya kufunga ndoa.
Songa nayo…
“Kwani Diana? Rais mwenyewe sio yule wa duniani?”
“Adela? Unatakiwa uvute subira mpaka tufike tunapokwenda ndio umuone Rais wako. Na hapa ninavyoongea yupo ikulu na maaskari wengi sana wanakusubiria uku wakipiga matarumbeta kwa shangwe.Majigambo! Yaani mimi mwenzako nilifaudu kweli sikutaka hata muda uishe lakini ndio hivyo tena kwa sheria za kichawi ni miezi miwili tu kuishi na rais wetu huyu na siku zako zikiisha ni lazima akukate sehemu zako za siri nakuzibandika kichwani mwake ili asizeeke mapema nakukuacha ukirudi katika kambi yako ulipotoka ya kichawi”
Diana alijiza maneno matamu nakuikuta mwili ukiwa katika shauku zima la kufika uko niendako, nilitamani na mimi niwe na huyo rais toka nilivyoambiwa.sikulijali kabisa swala la kukatwa sehemu za siri na tena na rais anayeheshimika duniani. Nikajipa moyo konde!
”Kwahiyo Diana huyo Rais anayajua mapenzi ennhhh?”
“We weee Adela! Kwa mapenzi kwa rais ndio umefika. Wewe ngoja ukifika utaona mwenyewe. Ndio maana nakwambia nilitamani sana muda uongezwe miezi miwili ni michache jamani kufaidi mapenzi na rais wetu huyu!”
Njia nzima Adela mimi nilikuwa kama nimemwagiwa maji tena yale maji yenye ubarafu ndani yake. nilikuwa mtu wa kusisimka ovyo kila nilivyotajiwa jina la rais. Nilijipa mawazo mengi sana.Mawazo ya kuishi maisha mapya na rais niliokuwa nikitamani sana kuwa naye. Mabinti wale warembo waliokuwa wamevalia nguo za dhahabu na meno yao ya ming’aro bado walikuwa nyuma yetu wakitusindikiza. Njiani tulipishana na wengine tena wengi na wote hakuna hata mmoja aliyetusemesha zaidi ya kuonesha sura za tabasamu. Tabasamu la kunipokea! Tuliendelea na safari ya kupita chini ya maji mengi kwa urefu kidogo bila hata ya kuchoka wala kuogelea. Tulikuwa tukitembea kawaida sana kama tukiwa nchi kavu tu. Mchawi yeyote anauwezo wa kutembea juu ya maji au ndani ya maji pasipo kulowana hata tone. Na yote huwa ni kwa nguvu za kichawi.
“Adela?”
Aliita Diana kwa utuli. Kimya! Akanikagua mwili wangu juu mpaka chini kisha akaninyooshea mkono upande wa pembeni yangu.
“Umepaona paleeee?”
“Ndio kwani kuna nini Diana?”
“Pale wanapopiga matarumbeta ndipo kuna rais ambaye anakusubiri mfunge ndoa. Na wale wapambe wote ni mapolisi na mabodigadi wake. Unachotakiwa ni kunisubiri hapa hapa nikakuletee nguo za harusi upande ule.Nisubiri!”
Aliongea Diana na kuniacha nikiwa na maswali mengi kichwani. Macho yaliendelea kumuangalia Diana lakini akili haikuwa kwake. Nilibaki nikijiuliza moyoni.
“Inamaana ni ndoa ya kichawi au?”
Niliuchukuwa mkono wangu nikapiga kifuani kwa hasira. Upuuzi! Nikageuka nyuma na kutaka kutoroka niondoke zangu. Nguvu za kichawi! Kitendo cha kuinua mguu tu nakugeuza nikashangaa nyao zikibaki chini kama ilivyowahi kunitokea hapo awali. Nikauinua na mguu mwingine nao ivyo ivyo. Nikaanza kuhisi maji yanaingia mwilini mwangu yakiniingilia kutokea chini ya miguu zilipobanduka nyayo. Mwili ukawa mrefu sana na mnene mithili ya mti wa mbuyu. Sikujali! Nikaanza kurudi nyuma nilipotoka. Kadri nilivyoanzisha spidi ndivyo na mikono yangu ilivyokuwa ikituna kwa kujawa na maji mengi. Mkono wa kushoto ukatuna sana maji ukapasuka nyang’anyang’a chini. Ukagawanyika vipande vipande. Sikutaa kuzubaa nikaendelea na safari ya kutoroka tena, nikashangaa mkono wa pili nao ukipasua vipande vipande nakuanguka mpaka chini.Mikono yangu yote ikiwa haipo. Nikabaki nikiongozwa kwa miguu pekee pasipo mikono. Kila hatua nilivyokuwa nikizidisha kupiga ndivyo na miguu nayo ilikuwa ikinivimba. Nikahisi nayo ikijaa maji nakutanuka kuwa mikubwa sana mithili ya mnyama tembo. Nguvu ya kukimbia sikuwa nayo tena, nikabaki natembea.Tena nikitembea ule mwendo mdogo wa mnyama ‘tembo’.
“Adela? Adelaaaaaaaaa??”
Nikasikia sauti ya Diana ikiniita kwa mbaali sana. Nikainama chini nakumuona Diana mdogo kama sisimizi. Nikasogeza sikio langu kumsikiliza. Akapanda na kulishikilia sikio langu. Nikainuka naye akiwa kaning’inia kwenye sikio langu la upande wa kushoto.
“Adela, nini tena unataka kufanya?. Hili ni zaidi ya eneo la kichawi na kamwe usijaribu kutoroka kabisa!. Rais amekasirika sana baada ya kuona unataka kumkimbia. Na hajaamini kama kweli umeshalala na maiti ishirini. Hakuamini tena na akikasirika zaidi utarudi tena duniani ukachomwe moto na watu wa duniani wasiotupenda tuwe wachawi.”
Maneno ya Diana yaliuchoma sana moyo wangu. Diana akajishikiza karibu na pua yangu nakuteremka mpaka kwenye lipsi ya mdomo wangu uku akipishana na machozi yaliokuwa yakianza kunibubujika. Akatumia mikono yake kuutanua mdomo wangu. Akadumbukiza dawa ndani yake. Dawa yenye nguvu za kichawi.Akatoka mpaka nje nakudondoka chini. Ile dawa ikanifanya nijisikie kizungu zungu kwa muda nikiweweseka. Nikadondosha limwili langu mpaka chini nakuanza kunywea nakurudi katika mwili wangu ulivyo kuwa. Nikawa mdogo
“Adela?”
“Ndio Diana”
Sikuamini kama ndani ya ule muda mfupi nilikuwa nimerudia katika ile hali yangu ya Adela yule wa zamani. Viungo vyangu vyote vilikuwa vimeshajikusanya nakuwa Adela mpya aliokamilika viungo vyote. Diana akanikabidhi nguo nzuri na za kung’aa. Nikazivaa kisha akanipa saa na pete inayong’aaa vyote vikanipendeza sana.
“Tanua mdomo Adela?”
Nikatanua, Diana akaniweka meno ya bandia. Yale meno yenye mng’aro wa silva.Nikametameta! Diana akanishika mkono nakuongoza tena tulipokuwa mwanzo pale ambapo niliona umati wa watu kwa mbali ukisherekea kwa matarumbeta. Ambapo Diana aliniambia kuwa rais ananisubiri tufunge ndoa. Mikononi walinipa nishike kichwa cha binadamu tena cha mtoto mdogo ikiwa ni ishara kama ua. Gauni langu lilikuwa lakumetea meta sana hali iliyofanya kule kumetatmeta kushindane na mwanga wa maji. Hatimaye baada ya hatua kadha tukawa tumeshafika eneo ambalo rais alikuwa akinisubiria kwa hamu.
“Adela, rais huyo hapo anakuja kukuchukuwa mpokee na mpige busu uondoke naye!”
Aliongea Diana kwa kunong’ona kupitia sikioni mwangu. Macho kodo! Sikutaka kuhamini.
“Jesus!”
Hakuwa rais yule wa duniani niliyemdhania bali alikuwa ni rais wa wachawi. Mwili wake mkubwa na weusi uliopitiliza mithili ya dikteta yule wa zamani wa Uganda ‘Idd Amin’. Minyamanyama ya mwili wake ikanifanya kuogofya sana. Mwili wake ulikuwa umezungukwa na vichwa vya watoto wachanga zaidi ya thelathini tena vikitoa machozi kwa kulia kwa uchungu. Macho yake yalikuwa na rangi tofauti tofauti. Yalikuwa yakibadilika kama taa za disco kila alipokuwa akinisogelea. Kichwani hakuwa na nywele hata moja zaidi ya kuwa na manundu manundu na aliponikaribia karibu zaidi ndipo nikagundua kuwa kichwani kuna sehemu za siri za wanawake wengi zimeganyanyika gawanyika. Akanifikia karibu.
“Adela mke wangu mpya!”
Aliongea kwa sauti ya kutetemesha hali ilionifanya mwili kudhoofu kwa muda. Mkono wake ulikuwa umenakshiwa kwa midomo ya watu wa duniani. Nikageuka nyuma kumuangalia Diana.Patupu! hakukuwa na Diana na hata wale watu wapambe pembeni walikuwa kama wameganda kwa mshangao mithili ya mtu aliyeganda kwenye barafu.
“Mimi ndiye rais wa wachawi wote hapa Tanzania na leo nipo na mwanamke mzuri kama wewe. Nipo tayari kufunga ndoa na wewe. Kwanza nataka kuona utamu wako Adela!!”
Akaendelea kuongea kwa sauti ya kukwaruza na ya kiubabe. Akanishika mkono mpaka katika eneo kubwa lililokuwa limekaa mithili ya kitanda. Lakini ilionesha kuwa kitanda kimetengenezwa kwa kutumia ngozi ya binadamu hawa wa duniani. Akanilaza mpaka kwenye hicho kitanda. Akavua ngozi ya binadamu ambayo alikuwa amejiziba eneo la sehemu za siri. Tahamaki! Macho yangu yakakutana na mioyo ya watoto wachanga mingi mingi ikiwa imezunguka kwenye sehemu zake za siri uku uume wake ukionekana kwa mbali sana. Akanilalaia kwa juu nakutoa ulimi ambao nao ulikuwa umetanda kucha kucha hizi za bandia ambazo wanapenda kuzibandika sana kinadada wa duniani.
*********************************
**** Huyo ndiye Rais wa wachawi ambaye Adela aliandaliwa aje kuolewa naye! Na tayari rais anataka afanye naye mapenzi ndio afunge ndoa, Rais atafanikiwa kufanya mapenzi na Adela? Na huwa anafanya vipi mapenzi akiwa na mwili wa dizaini hiyo?
***** Nini hatma ya Adela katika maisha yake ya kichawi? Ataweza kuishi na Rais? Na kama atashindwa maisha yatakuwaje kwake?
**** LIKE na SHARE nyingi zinasaidia kuifanya simulizi hii inoge na kuwa tamu zaidi. Gonga LIKE yako na SHARE simulizi hii.
***** Usisahau kutuma neno ‘MAITI 20’ inbox hapa uwanjani halafu nitakupa simulizi yote mwanzo mpaka mwisho kwa gharama ya chini kabisa ya shilingi 2500/= tu. Tuma pesa yako kupitia namba. Kwa wale wan je ya nchi wani inbox niwape maelekezo jinsi ya kuipata.
Tigo: 0713 133633 – Andrew Andrew
Voda: 0758211153 – Bahia.
:::: ANGALIZO :::
Nashukuru kwa wale wote ambao tulikuwa pamoja kuanzia mwanzo wa simulizi hii mpaka sehemu ya hapa nasema asanteni sana kwa kuguswa na simulizi hii. Hakika baadhi yenu mmekuwa katika wakati mgumu pindi mlipokuwa mkisoma. Napenda kuwajulisha wote kuwa simulizi hii hapa ilipofikia ni parefu sana kwa kusoma bure bila kulipia gharama yeyote. Hivyo basi simulizi hii kuanzia leo haitakuwepo tena hapa uwanja wa simulizi. Na kama utahitaji utumiwe basi usisite kutuma pesa yako katika namba zangu hapo juu na utatumiwa simuilizi yote ikiwa mwanzo mpaka mwisho kabisa.
Tags
HADITHI NA RIWAYA