USAJILI: KEVIN STROOTMAN AENDI POPOTE MSIMU HUU - ASEMA MKURUGENZI WA PSV

clip_image002Mkurugenzi wa michezo wa PSV Marcel Brands ameweka wazi kwamba klabu yake haina mpango wowote wa kumuuza  Kevin Strootman kuelekea msimu mpya wa 2013-14 .
Kiungo huyo wa kiholanzi kwa muda mrefu sasa amekuwa akihusishwa sana na uhamisho wa kwenda Manchester United, wakati klabu ya Napoli pia imeonyesha nia ya kumhitaji kiungo huyo mwenye miaka 23.
"Hatutaki kumuuza Strootman msimu huu. Anajua kwamba kwamba atabaki PSV kwa msimu mwingine," Brands aliiambia De Telegraaf.
Strootman ni zao la academy ya Sparta na pia alishawahi kuvaa jezi ya klabu ya Utrecht kabla ya kujiunga na PSV mwaka 2011. Tangu wakati huo ameimarika na kuwa mmoja wa viungo bora bora chipukizi barani ulaya.

Ana mkataba na PSV unaodumu mpaka mwaka June 2016.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post