DROGBA KUMBE 'DHULUMATI', MAHAKAMA YAMKUTA NA HATIA NA KUMUAMURU ALIPE EURO 450,000

clip_image003Didier Drogba

MAHAKAMA Ufaransa imemuagiza mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba kulipa Euro 450,000 kwa kampuni ya ujenzi ya mjini Corsica baada ya kutoilipa kwa kumfanyia kazi mjini mjini Abidjan.

Kampuni ya Acqua Viva ilimfikisha kortini mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea Mei kwa kugoma kulipa salio la malipo baada ya kujengewa nyumba ya kifahari iliyokamilika mwaka 2009.
Kampuni hiyo imelalamika pia wafanyakazi wake kuzuiwa kufika eneo la nyumba hiyo waliyojenga, kitu ambacho Jaji amesema si haki na kwamba kilitokana na maelekezo ya Drogba na mkewe, raia wa Mali, Lala Diakite.

Wakati mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 35, aliyejiunga na Galatasaray ya Uturuki mapema mwaka huu, ameamua kukata rufaa, lazima alipe fedha hizo mapema ili kutekeleza amri ya Mahakama.

SOURCE: SUPERSPORT.COM

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post