RYAN GIGGS ATANGAZWA KUWA KOCHA MCHEZAJI MAN UNITED

clip_image001Manchester United imewatangaza Ryan Giggs kama kocha mchezaji na Phil Neville kuwa katika jopo la makocha.

Giggs, atatimiza umri wa miaka 40 mwezi Novemba na mchezaji mwengine wa zamani Neville mwenye umri wa miaka 36,amekuwa wa mwisho kutangazwa na meneja mpya David Moyes katika jopo la makocha wa Manchester United.

"Nimefurahishwa sana na kwamba Ryan amekubali bahati ya kuwa mchezaji kocha"amesema Moyes.

Neville,amechukuwa nafasi iliyoachwa Rene Meulensteen, ambaye alijiunga na Guus Hiddink meneja wa sasa wa club ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post