Kocha mwenye maneno mengi nchini Jamhuri Kihwelo 'Julio' amepewa mkataba mpya na simba wa mwaka mmoja baada wa ule wa awali wa miezi 6 kuhitimishwa hapo juzi.
Julio ataendelea kuwa msaidizi wa Abdalla Kibaden baada ya kupewa mkataba mpya na uongozi wa Simba SC utakao muweka katika benchi la ufundi la simba mpaka mwakani mwezi huu.
Akizungumza na moja ya redio hapa nchini hii leo Julio alisema kuwa anashangazwa na vyombo vya habari vilivyo ripoti kuwa hana chake ndani ya Simba SC, wakati mkataba wake wa awali ukikimbilia kuisha.
Julio alisema kuwa amesaini Simba mkataba wa mwaka mmoja na anamini atafanya kazi kubwa chini ya Abdallah King Kibaden Mputa katika kuliongoza benchi la ufundi la Simba SC.
Julio alisema kuwa wanataka kuwazodoa wale wanaosema makocha wazawa hawawezi fanya vizuri, na kuwataka mashabiki wangoje kuona kazi inayofanywa na Kibadeni na yeye ndani ya Simba SC.
Tags
SPORTS NEWS