NI VITA TENA KATI YA MAKOMANDOO NA ALLY KIBA, STYLE YA KIBABA BABA INAHUSIKA

clip_image002Kama unakumbuka miezi kadhaa iliyopita Kundi la Makomando lilitambulisha style ya dancer maarufu kama Kibega na baadae tulisikia kuwa ni style ya bendi nyingine hapa Tanzania. Well kitu hiki kimetokea tena. Sasa ni Makomando na Ali Kiba.

Nimefanya Exclusive interview na Makomando wamefunguka kuhusu style yao mpya ya kucheza ya Ki-BabaBaba inayochezwa kwenye Wimbo wao mpya wa Ki-BabaBaba.

Makomando wamesema tayari Msanii Mwenzao Ali Kiba amewapigia simu nakusema hii style ni yake na hataki waitumie. Kwa mujibu wa Makomando wamesema Ali Kiba amewauliza kwanini wametambulisha style yake ya kucheza na kuwa dancers wa Kiba [ 4 Real Dancers ] ndio wamewafundisha Makomando style hio.

Makomando wapo kwenye harakati za kusajili style hii mpya ya KiBabababa leo au kesho, wanataka kusajili Basata ili Msanii au bendi yoyote isidai kuwa ni style yao.clip_image001Ali Kiba Amesema alipo Ona wanatambulisha style hio, alichofanya nikuwapigia simu nakuwa tahadharisha kuwa wanatumia style ya Dancer Wake na kuwa walikuwa na mpango wakuitumia kwenye video yake.

Ali aliendelea kusema Makomando walimbishia na kusema Style hio ni yao, yameigundua na wameipa jina, waka mkatia Kiba simu.

Ali kiba amesema amekasirishwa na kitendo cha kubishiwa kuhusu style hio na kukatiwa simu na wasanii anao waona kama wadogo zake.

Fahamu Ali Kiba na Makomando wote wana mpango wakutumia style hio kwenye video zao.

Source: Sammisago.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post