Unknown Unknown Author
Title: WENGER AWEKA MSISTIZO KUMSAJILI ROONEY, ASEMA HATANII HATA KIDOGO NA PIA FABREGAS ANAMRUDISHA NYUMBANI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtafutwaji: Wayne Rooney inaaminika anataka kuondoka Manchester United Cesc Fabregas aliondoka Arsenal kwenda Barcelona  mwaka 2011 KOCHA A...

clip_image001Mtafutwaji: Wayne Rooney inaaminika anataka kuondoka Manchester Unitedclip_image001[6]Cesc Fabregas aliondoka Arsenal kwenda Barcelona  mwaka 2011

KOCHA Arsene Wenger amesema hana mzaha na hatabadlisha mawazo katika suala la kumsajili mshambuliaji 'aliyetikiswa' Manchester United, Wayne Rooney.

Nyota huyo wa England, ambaye alifunga bao zuri katika sare ya 2-2 dhidi ya Brazil usiku wa jana, ameonyesha nia yake ya kuondoka Manchester United msimu huu.

Mwezi uliopita, kutoka Sportsmail ililipua habari kwamba Arsenal wako tayari na wanajiamini watavunja rekodi yao ya dau la usajili kumsajili Rooney.

Na Wenger ametilia msistizo kauli yake, akisema yuko tayari kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

"Rooney anaweza kuwa mchezaji anayemvutia kila mtu duniani, nani anayeweza kumpiga chini yeye?" Wenger aliiambia Al Jazeera.

Wenger pia anataka kumrejesha Nahodha wake wa zamani, Cesc Fabregas Emirates na anaamini kiungo huyo anaumizwa na kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha Barcelona.

Katika Mkataba wake wakati anaondoka Emirates kwenda Nou Camp mwaka 2011, ilikubaliwa Arsenal iwe klabu ya kwanza kupewa nafasi ya kumsajili Mspanyola huyo kwa dau la Pauni Milioni 20, lakini kiwango kinachotakiwa sasa ni Pauni Milioni 25 kama ada ya uhamisho wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top