Soma yote juu ya hii: Gazeti la michezo la kila siku la Catalan, Sport limeandika kwamba Barcelona inataka kumnunua kwa Euro Milioni 20 Torres
HAWATOSHI Messi na Neymar peke yao kuongoza safu ya ushambuliaji, Barcelona imeripotiwa kutaka kumnunua mshambuliaji Fernando Torres.
Gazeti la kila siku la Catalan, Sport limeandika kwamba Barcelona inataka kutoa Pauni Milioni 17 (zaidi ya Euro Milioni 20) kumnunua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anayekipiga Chelsea.
Msimu | Mabao |
2012-13 | 22 |
2011-12 | 11 |
2010-11 | 10 |
2009-10 | 22 |
2008-09 | 17 |
Pamoja na hayo, Torres hatakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza bali atakuwa anatokea benchi kama super-sub.
Matumani ni kwamba, Torres atatengeneza uzito sawa na aliokuwa nao Henrik Larsson, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki enzia zake Nou Camp kwa kufanya vitu adimu akitokea benchi hususan alipotoa pasi za mabao yote Barcelona ikishinda 2-1 dhidi ya Arsenal katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2006.
Lakini Sport limemsifia Torres ni mshambuliaji wa uhakika ambaye anaweza kufunga mabao kati ya 20 na 25 kwa mwaka.
Bao la ushindi: Torres alifunga dhidi ya Barcelona Uwanja wa Nou Camp katika Nusu Fainali ya Mabingwa mwaka jana
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.