Bale yupo mapumzikoni Amerika, lakini anatakiwa na PSG, pamoja na kocha wake, Villas-Boas
KLABU ya Paris Saint-Germain inajiandaa kuipiga bao Real Madrid kwa kumwaga Pauni Milioni 85 kumsaini Gareth Bale.
Mabingwa hao wa Ufaransa, wanamtaka kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas na wanatumai wakimnasa awe kocha wao mkuu, itasaidia pia kumkamata kwa urahisi Bale, kwani atashawishiwa na kocha wafuatane Paris.
Pamoja na hayo, hata kama kocha Villas-Boas ataamua kubaki London, hawataacha mkakati wao wa kumsaini Bale kwa kulipa ada kubwa ya uhamisho.
PSG imetumia zaidi ya Pauni Milioni 200 kwa ada za uhamisho wa wachezaji tangu mwaka 2011 ilipochukuliwa nma mabilionea wa Qatar Sport Investments, kampuni inayomilikiwa na familia ya kifalme Qatari, na tayari wanataka kuvunja rekodi ya dunia ya usajili kwa kumsajili Bale kutoka Tottenham.
Kwa sasa rekodi ya dunia ya ada ya uhamisho wa mchezaji ni Pauni Milioni 80, ambazo Real Madrid ilitoa kumnunua mchezaji wa Manchester United wakati huo, Cristiano Ronaldo.
Mkurugenzi wa Michezo wa Real, Zinedine Zidane alisema: "Ikiwa klabu yoyote itakwenda kutoa ofa Spurs, itagharimu fedha nyingi, labda hata kuvunja rekodi ya usajili. Kuna klabu nne au tano ambazo zina uwezo wa kifedha, lakini si uvunja rekodi ya usajili kiasi hicho,".
Hizo ni pamoja na PSG, ambayo rais wake Nasser Al-Khelaifi, mwenye umri wa miaka 39, anayeiwakilisha familia ya kifalme Qatari na mchezaji wa zamani wa kulipwa wa Tenisi, yuko tayari kupambana na ofa yoyote itakayotolewa na Real.
Bale amekuwa babu kubwa msimu huu, akifunga mabao 26, aking'ara kwa kasi yake kubwa uwanjani kiasi cha kuwa bidhaa adimu katika kipindi hiki cha usajili cha majira ya joto.
Bale mwenyewe yupo mapumzikoni Florida na inafahamika na anasikilizia mustakabali wake. Anaishi na mpenzi wake Emma Rhys Jones na mtoto wao wa kike wa miezi nane, Alba Violet na angefurahi kubaki London kama Tottenham itaendelea kuwa katika mwelekeo sahihi.
Bale akionyesha uwezo wake Busch Gardens huko Florida, Marekani Bale akiwa Cheetah Hunt, Busch Gardens, Tampa, Florida
Bale atasikilizia hatima yake kujua wapi atakwenda kati ya PSG, Real na Manchester United kutokana na Tottenham itakapoamua kumuuza.
Kocha Villas-Boas anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Mwenyekiti Daniel Levy na anaweza kuamua kubaki iwapo atahakikishiwa bajeti nzuri ya usajili.
Mreno huyo amekuwa na wakati mzuri White Hart Lane, lakini inafahamika wanatakiwa kutumia fedha kwa kusajili wachezaji wazuri wenye uwezo wa kushindana katika Ligi ya Mabingwa na kushinda mataji.
Inafahamika, Villas-Boas anatazamia kuboresha kikosi cha Spurs, kwa kumsajili winga wa Barcelona, Ibrahim Affelay.
Zidane anataka kushindana na PSG kuwania saini ya Bale
Wakati huo huo, Villas-Boas anataka kuwauza Jermain Defoe na Scott Parker. Spurs pia inataka kumuuza Emmanuel Adebayor anayelipwa Pauni 100,000 kwa wiki sambamba na Tom Huddlestone na Benoit Assou-Ekotto.Parker, Adebayor na Assou-Ekotto wote wataondoka White Hart Lane
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.