BAADA YA KUMTUKANA WAZIRI MKUU,HATIMAYE SUGU AOMBA MSAMAHA

clip_image002Mhe Suguclip_image002Waziri Mkuu, Mhe. Pinda
BAADA ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia,
Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu amemuomba radhi mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa akiwaomba radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba Tanzania haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu watanzania, naombeni radhi kwa tusi nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio langu kumtukana mmoja wa viongozi wa nchi."

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post