MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YAFUTWA, KUSAHIHISHWA UPYA–MH. LUKUVI

Habari kutoka bungeni ni kwamba matokeo yote ya  kidato  cha  nne yamefutwa na yatasahihishwa upya haraka iwezekanavyo..

Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato  cha nne  imesomwa  bungeni  leo  na  mh.LUKUVI.

LUKUVI amesema sababu zilizosababisha  wanafunzi  wafeli   ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa  na  utaratibu  mbovu  wa  baraza  la  mitihani  uliotumika  bila  kuwashirikisha  wadau  wa  elimu

Mh.  LUKUVI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS. ...

Hivyo  basi, matokeo  hayo  YAMEFUTWA na  YATASAHIHISHWA  UPYA

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post