RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA JUMA LA MAJI KITAIFA-LINDI

Rais Jakayo Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha sherehe za kuadhimisha Juma la Maji Kitaifa zitakazofanyika tarehe 22 mwezi huu Mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia kwa waandishi wa habari, inaeleza kuwa uzinduzi wa shereehe hizo utafanyika katika kijiji cha Mtandi wilaya ya Kilwa taraehe 16 ambapo kilele chake kitaendeshwa uwanja wa Ilulu katika Manispaa ya Lindi.
Simbakalia amesema madhimisho hayo ya juma la maji mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo ''Mwaka wa Ushirikiano wa Maji Kitaifa" ukiwa na madhumuni ya kuelimisha wananchi kuhusu sera ya maji na majukumu yao katika kuitekeleza.
Amebainisha kuwa madhumuni hayo yanalenga kuborehsha utaoaji wa huduma ya maji, usafi na uhifadhi wa mazingira pamoja na usimamizi na utunzaji wa rasilimali za maji nchini kote.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post